Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema Ziwa Tanganyika ni Urithi wa Dunia hivyo linapaswa kulindwa na kutunzwa kwa ajili ya urithi wa vizazi vijavyo.
Mhe. Andengenye ametoa Rai hiyo alipozungumza wakati akifungua Kikao cha wadau kutoka nchi jirani za Congo DR, Burundi, Zambia, Rwanda na mwenyeji Tanzania, kilicholenga kuweka mikakati ya pamoja katika kulinda uthamani wa Ziwa Tanganyika kilichofanyika mkoani hapa.
Amesema ziwa hilo linahudumia zaidi ya watu Mil.12 kupitia usafiri, uvuvi sambamba na shughuli nyinginezo za kibinadamu ikiwemo upatikanaji wa huduma ya Maji.
Amesisitiza uchukuliwaji wa hatua madhubuti kupitia maazimio yatakayotolewa na wajumbe wa kikao hicho ili kudhibiti uharibifu wa Mazingira na matumizi yasiyo sahihi kwa lengo la kuepuka kupoteza sifa na thamani ya ziwa hilo.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wajumbe wa kikao hicho kuwa mabalozi wazuri wa kuhamasisha wananchi katika maeneo yao kuacha kufanya shughuli zinazokinzana na zoezi zima la utunzaji wa mazingira ili kulinda uoto na maji yanayoendelea kujaza ziwa hilo.
‘’Mto malagarasi unachangai zaidi ya Asilimia Sabini ya Maji yanayoingia katika ziwa Tanganyika hivyo tunapaswa kutoa elimu kwa wananchi kuepuka kuharibu mazingira sambamba na vyanzo mbalimbali vya mito inayochangia maji katika ziwa’’ amesisitiza Mkuu wa Mkoa.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa