CLINTON JUSTINE-KIGOMA RS
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Baloz.i Simon Sirro ameagiza kufanyika upya kwa Tathmini ili kuwabaini na kuwafidia wakazi waliokutwa wakiishi eneo hilo na mwekezaji ambaye ni Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum kiuchumi Tanzania (TISEZA) katika Shamba Namba 206 Lugufu lililopo kijiji cha Mwamila Kata ya Kazuramimba wilayani Uvinza mkoani Kigoma kwa lengo la kutatua mgogoro uliopo baina ya taasisi hiyo na wananchi wanaoishi ndani ya eneo hilo la uwekezaji.
Balozi Sirro ametoa kauli hiyo alipokutana na wakazi wanaoishi ndani ya shamba hilo na kuuelekeza uongozi wa Halmashauri ya Uvinza kufanya upya tathmini ili kubaini iwapo wakazi hao walikutwa wakati likifanyika zoezi la kutenga eneo la shamba hilo ili waweze kulipwa fidia waweze kupisha katika eneo hilo.
Amesema serikali ya Tanzania haipo tayari kushudia wananchi wakiwa wazururaji ndani ya nchi yao huku akitoa maelekezo kwa uongozi wa halmashauri kuwaacha wakazi hao kuendelea na majukumu yao ya ufugaji na kilimo katika eneo hilo huku mwekezaji akisubiri yafanyike mapitio kisha kutolewa uamuzi wa serikali.
Kantate Julius Mkazi wa kijiji cha Mwamila amesema baadhi yao wamekua wakiishi kna kufanya shughuli za ufugaji na kilimo katika Shamba hilo tangu mwaka 2010 huku wakiwa wamepanda mazao mbalimbali ya kudumu na kuiomba serikali iwatengee eneo lingine ili waweze kumpisha mwekezaji.
Shamba hilo lenye ukubwa wa Hekta 10,529.96 linamilikiwa kwa makubaliano ya upangishaji wa muda mrefu na Mamlaka ya uwekezaji TISEZA kwa ajili ya Kilimo na Ufugaji.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa