Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Mkandarasi mjenzi wa Reli ya kisasa ya SGR kipande cha Uvinza-Msongati Burundi, Yu Chao (wapili kushoto) Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa, (wapili kulia) Mwakilishi kutoka Shirika la reli la China Hu Bo ( wakwanza kushoto) pamoja na Bwana Lin Xiaotong.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amekutana na kufanya mazungumzo mafupi na mwakilishi wa Mkandarasi mjenzi wa Reli ya kisasa (SGR) Kipande cha Uvinza hadi Msongati nchini Burundi, Yu Chao aliyefika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa lengo la kujitambulisha.
Kupitia mazungumzo yao, Balozi Sirro amesema serikali ya mkoa ipo tayari kutoa kila aina ya ushirikiano ili kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa ufanisi kama ilivyopangwa na Serikali.
Aidha, Sirro ametumia fursa hiyo kuwaalika wawekezaji kutoka china ili kuwekeza mkoani Kigoma hususani katika eneo maakum la uwekezaji la mkoa, (Kigoma Special Economic Zone) kutokana na uwepo wa
fursa nyingi za kibiashara na uhakika wa masoko katika nchi za Congo DR na Burundi.
Upande wake Yu Chao, ameipongeza Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa kufanikiwa kutekeleza mradi wa ujenzi wa reli ya SGR ambao unamchango mkubwa katika kuendeleza sekta ya uchumi kupitia usafirishaji.
Amesema mradi wa ujenzi wa reli hiyo kwa kipande cha Uvinza hadi Msongati Burundi Km. 240, utachochea uchumi na kuongeza ushirikiano wa kimaendeleo baina ya nchi ya Tanzania na Burundi.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa