Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali (Mstaafu) Emmanueli Maganga, amagiza kusitishwa maramoja shughuli za Kilimo katika msitu wa Kagerankanda, wakati Uongozi wa Mkoa ukikamilisha mipango na taratibu za Ugawaji wa sehemu ya eneo la msitu huo lililotolewa kwa wakulima na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Amewaagiza wataalamu wa na Uongozi wa Wilaya na Halmashauri ya Wilayani Kasulu kuharakisha taratibu za kubaini na kupima sehemu ya eneo la msitu wa Kagerankanda ili wananchi waweze kugawiwa na kuanza shughuli zao za kilimo.ametoa maagizo hayo wakati akizungumza katika Kikao cha Madiwani na watendaji Wilayani Kasulu.
Mhe. Maganga ametoa maelekezo hayo Wilayani kasulu ikiwa ni utekelezaji wa tamko la Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa wakati wa ziara yake Mkoani Kigoma tarehe 21 Juni, 2017 ambapo alisema kuwa wananchi wapatiwe maeneo katika sehemu walizokuwa wanalima msitu wa makere. Ruhusa ya kulima eneo hilo haimpi mwanchi kuvuka mipak.
Amewataka Wanasiasa waache kuwadnganya wananchi kuwa wao ndiyo waliomshawishi Rais kutoa eneo hilo "Hakuna mtu aliyemshawishi mhe. Rais kutoa eneo hilo kwa wananchi bali huo ni utashi wake na mapenzi yake kwa wananchi wa Kasulu hivyo waache kujitafutia umaarufu kwa kuwadanganya wananchi" alisema Maganga.
Ikumbukwe kuwa msitu wa Kagerankanda limekuwa likiharibiwa kwa shughuli za kilimo kutokana na ardhi ya eneo hilo kuwa na rutuba na hali ya kustawisha mazao kwa wingi na kwq uhakika. Tangu miaka ya 1990 hadi sasa eneo hili limekuwa likivamiwa na wananchi kiholela.
Amewaeleza kuwa baada ya kaati kumaliza kazi za kupima na kubaini mahitaji ya Ardhi kulingana na eneo litakalotolewa taratibu za kugawa zitazingatia sheria ya Ardhi namba 4 & 5 ya mwaka 1999.Ameagiza kwasasa eneo hilo lipo chini ya serikali, mwananchi haruhusiwi kujimilikisha maeneo hayo mpaka baada ya kugawiwa.
Wanachi wametahadharishwa kuwa baada ya kupata mgao wa maeneo mwananchi atakayevuka alama za mipaka zitakazowekwa serikali haitamvumilia. Ndugu zangu viongozi na wanasiasa tushirikiane kutoa elimu kwa wananchi, tuheshimu na kuthamini huruma na upendo wa Mhe. Rais kwa kuruhusu sehemu ya eneo la msitu wa Kagerankanda kugawiwa kwa wakulima wa kasulu. Kufuatia tamko la Mhe. Rais jumla ya ekari10 elfu zitagawiwa kutoka msitu wa Kagetankanda wenye jumla ya ekari 72 elfu kwa sasa.
Matumizi ya vibarua wanaajiriwa na watu wanaolima mashamba makubwa katika eneo la msitu Kagerankanda matokeo yake vibarua hao wanajipatia mashamba na kumiliki maeneo kinyume na utaratibu. Mhe. Mkuu wa Mkoa amewataka wanaotumia vibarua toka nje ya nchi kufuata taratibu kanuni na sheria kuwapata vibarua hao.
Maeneo yatatolewa kwa vijiii husika zinazozungunga eneo hilo, halmashaui na uongozi wa wilaya utazingatia vigezo na taratibu za kugawa. Kwa upande wao voongozi mbalimba wameeleza kuwa uvamizi wa msitu wa makere kweli unasababishwa na wanasiasa wanaojinadi kuwa wao ndiyo wanaoweza kushawishi msitu huo uweze kutumika kwa kilimo, wameiomba serikali iwasaidi kuwaonya wanasiasa wenye mawazo ya uharibifu wa rasilimali za Taifa.