Kituo cha utafiti wa zao la michikichi kitajengwa Mkoani Kigoma katika eneo lililopo Kihinga nje kidogo ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, lengo ikiwa ni kufufua na kuendeleza kilimo cha zao hilo ambalo lilisahaulika kwa miaka mingi.
Maamuzi haya yametolewa na Waiziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa(Mb) wakati alipofanya Mkutano Mkubwa wa Wadau wa zao la Michikichi na kukagua mashamba ya Michikichi na shughuli mbalimbali zinazohusiana na mnyororo wa thamani wa zao la Michikichi.
Mheshimiwa Waziri Mkuu alisema lengo la ziara yake MkoaninKigoma ni kutoa msisitizo na msukumo kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma ili kufufua na kuendeleza Kilimo cha zao la Michikichi. Zao la michikichi Mkoani Kigoma na kuahikisha zao hilo limepewa nafasi ya kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi kwani ndilo zao litakaloufanya mkoa wa Kigoma kungāara katika sekta ya viwanda.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
HakimilikiĀ©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa