• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko / Mrejesho |
KIGOMA   REGION
KIGOMA   REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Kigoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Seksheni ya Elimu
      • Seksheni ya Afya
      • Seksheni ya Miundombinu
      • Seksheni ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Mipango na Uratibu
      • Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Fedha
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwami
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Kibondo
      • Halmashauri ya Kibondo
    • Wilaya ya Kigoma
      • Halmashauri ya Kigoma
      • Manispaa ya Kigoma Ujiji
    • Wilaya ya Kakonko
      • Halmashauri ya Kakonko
    • Wilaya ya Kasulu
      • Halmashauri ya Kasulu
      • Halmashauri ya Kasulu Mji
    • Wilaya ya Uvinza
      • Halmashauri ya Uvinza
    • Wilaya ya Buhigwe
      • Halmashauri ya Buhigwe
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Kigoma Ujiji
    • Halmashauri ya Buhigwe
    • Halmashauri ya Kasulu
    • Halmashauri ya Kasulu Mji
    • Halmashauri ya Kibondo
    • Halmashauri ya Uvinza
    • Halmashauri ya Kakonko
    • Halmashauri ya Kigoma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Kigoma Special Economic Zone
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mikakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Picha

Zao la Mchikichi linavyoweza Kuwanufaisha wananchi Mkoani Kigoma

Posted on: March 23rd, 2017

Michikichi ni zao mojawapo ya mazao ya mafuta ambalo hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Kigoma, Mbeya na Tanga hapa nchini Tanzania. Aidha zao hili hulimwa pia kwa kiasi kidogo katika mikoa ya Kagera, Pwani, Rukwa, Morogoro na visiwa vya Pemba na Unguja.Mkoa wa Kigoma ukiwa ni eneo muhimu kwa uzalishaji wa zao la michikichi hapa Tanzania kwa mwaka huzalisha zaidi ya tani 2,000 za mawese na zaidi ya tani 450 za mafuta ya mise. Zao la mchikichi limekuwa mkombozi kwa wakulima wengi wa Mkoa wa Kigoma kwani hutumika kwa chakula, biashara, mafuta ya mise hutumika katika mapishi ya vyakula mbalimbali pia husaidia mwili kupata nguvu na joto na hutumika katika utengenezaji wa sabuni na vipodozi mbalimbali. Hata hivyo nchi za Indonesia na Malaysia ambazo zilitoa mbegu ya zao la mchickichi kutoka Mkoa wa Kigoma nchini Tanzania miaka ya 1960 kwa sasa zinaongoza kwa uzalishaji na usambazaji wa mafuta ya mawese na bidhaa zitokanazo na michikichi. Malysia pekee huzalisha tani milioni 18.79 million za mafuta ya mawese na kusambaza tani milion 18 za mazao yanayotokana na zao la michikichi duniani yakiwemo mafuta ya mawese ambayo Tanzania imekuwa ikiagiza takribani asilimia 65 ya mafuta ya mawese kutoka nchini ya Malaysia, zikifuatiwa na nchi nyingine kama Kolumbia na Thailand. Kwa ukanda wa Afrika nchi za Nigeria, Kenya, Ghana, Cameroon na Benin zinatajwa kuongoza katika uzalishaji wa zao la mchikichi ambapo nchi ya Naigeria huzalisha tani milioni 2.3 ya mafuta ya mawese kwa mwaka na kuifanya kuwa nchi ya tatu kwa uzalichaji kidunia. Kiasi hiki ni kingi ukilinganisha na fursa na uaptikanaji wa zao hili nchini Tanzania hususan Mkoa wa Kigoma haipo katika rekodi ya uzalishaji. Sababu kubwa zinazofanya zao hili kutojulikana na hata kutomnufaisha mkulima wa kawaida nchini Tanzania ni teknolojia duni ya kilimo cha zao hili na ukosefu wa miunndombinu ya kuchakata mazao yatokanayo ya mchikichi hususan viwanda. Kwa upande mwingine wataalamu wa kilimo hawajaweza kutilia maanana juu ya umuhimu wa zao hili, Serikali nayo haijawea kipaumbele namna ya kutoa ruzuku kwa wakulima wa zao la mchikichi ili waweze kujikwamua kiuchumi. Kadhalika bidhaa mathalani vile mapaa ya ndani (ruffing Materials) ambayo hutokana na makapi ya mchikichi huingizwa kwa wingi nchini kutoka Malaysia, na Afrika ya Kusini. Wakulima wa zao hili wengi hutumia zana duni katika kuchakata mazao ya michikichi kiasi ambacho hakiwapi tija kukuza uchumi. Sambamba na ukosefu wa zana za kilimo nguvu ya serikali kupitia wizara ya Kilimo ingeweza kufikiri namna ya kuwashirikisha wadau wa maendeleo, mashirika binafsi ili kushawishi uwekezaji katika zao la mchikichi kwa Kuweka miundombinu kama nishati ya umeme kwaajili ya kujenga viwanda. Kwakuwa zao hili hutoa malighafi zaidi ya tatu ingekuwa fursa kwa wakulima kutengeneza wigo wa upatikanaji wa biashara za mazao ya mchikichi kama vile vipodozi, vyakula vya mifugo, sabuni na mafuta ya kupikia na bidhaa nyingine nyingi kadha wa kadha. Serikali kwa kutumia wataalamu wake katika ngazi mbalimbali ikiwemo Halmashauri, na ngazi mbalimbali za uongozi hazina budi kushirikiana na mashirika mbalimbali ya maendeleo katika kuhakikisha kuwa zao la michikichi linakuwa moja ya mazao makuu katika kukuza kipato na kuwaondolea umaskini wananchi wa mkoa wa Kigoma.


Matangazo

  • MAZOEZI KWA AFYA YAKO March 23, 2017
  • UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024 September 12, 2024
  • UJIO WA MADAKTARI BINGWA MKOANI KIGOMA November 12, 2018
  • Fomu ya Usajili wa Maonesho TBS Kigoma May 01, 2022
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • RC ANDENGENYE AKABIDHI VITENGO VITENGO VYA LISHE MKOA NA WILAYA UVINZA

    May 09, 2025
  • DCP NARCIS MISSAMA AFANYA ZIARA MKOANI KIGOMA

    May 07, 2025
  • JAJI ASINA AKAGUA ZOEZI LA UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI-KIGOMA

    May 03, 2025
  • VYAMA VYA WAFANYAKAZI VISIGEUKE MAHAKAMA ZA KUWAHUKUMU WATUMISHI-RC ANDENGENYE

    May 01, 2025
  • Ona vyote

Video

RC ahimiza wananchi anuani za Makazi
Video nyingine

Tovuti zinazo fanana

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA BUHIGWE
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KAKONKO
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
  • HALMASHAURI YA MJI KASULU
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBONDO
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA
  • HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGOMA UJIJI
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA

Tovuti zinazo husiana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI PORTAL
  • IKULU
  • OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    MKOA WA KIGOMA

    Anuani: S.L.P 125

    Simu: 0282802330

    Simu ya kiganjani: +255766853404

    Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://bachelorthesiswritingservice.com

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa