Raia hao ambao wengi wao wanatoka maeneo ya Fizi na misisi Kivu kusini mwa Congo wamedai kuwa Vikosi na wapiganaji wa maimai nchi Congo na vikundi mbalimbali vya waasi vinavyoendelea kupigana nchini vimewatia hofu na hivyo kuanza kukimbia nchini Tanzania kuomba hifadhi ya ukimbizi.
Wakizungumza mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Kigoma iliyotembelea katika kituo cha kupokelea waomba hifadhi kijiji cha Kigadye raia hao walisema sababu iliyowafanya kukimbilia Tanzania ni hofu ya usalama wa maisha yao kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya vikundi vya waasi na Serikali iliyopo madarakani.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali (mst.) Emannuel Maganga akiongoza kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa amesema tayari Mkoa umefika kuwaona raia hao na wanafana jitihada za kuhakikishah wanapatiwa huduma muimu za kibinadamu zinaboresha katika eneo hilo wakati kamati ya taifa ya kusikiliza maombi ya ukimbizi inajiadaa kuwasikiiza raia hao.
Kutokakana na wimbi kubwa hilo huduma za kibinadamu ikiwemo chakula, malazi zinahitajika haraka ili kuwahudumia raia hao ambao wengi wao ni kinamama na watoto.
Baadhi ya raia waliokimbilia nchini Tanzaia wamedai kuwa kutokana na kuahirishwa Uchaguzi Mkuu uliopaswa kufanika Desemba, 2017 dalili za kuzuka kwa mzozo wa mapigano uenda ukawaathiri amani nchini Congowa, Vyama vya upinzanu vimeanza kuonesha dalili za kupinga kusitishwa kwa uchaguzi, wamehofia amani.
Kituo cha kigadye wilayani kasulu, huenda kikashindwa kihimili idadi kubwa ya raia wa Congo wanaoendelea kfika kituoni hapo kwa madai ya kukimbia vita nchini mwao. Kusini mwa Congo kumekuwa na matukio ya hivi karibuni mashambulio ya mara kwa mara yanayosabisha hofu ya machafuko kwa wananchi.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa