Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa amekutana na kufanya Kikao kazi na watendaji wa Serikali Idara ya Ardhi mkoani Kigoma kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa Maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusu utatuzi wa migogoro ya matumizi ya Ardhi katika vijiji 975 Tanzania Bara.
Kupitia kikao hicho Waziri Silaa amewasisitiza watendaji hao kuongeza kasi katika kutatua migogoro hiyo bila kujali changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utekelezaji wa majukumu yao.
Aidha Waziri Slaa amewapongeza watendaji hao wa Umma kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya serikali mkoani hapa kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Masala amesema mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa iliyoguswa na maagizo ya Baraza la Mawaziri ikiwemo kuondolewa kwa baadhi ya vijiji katika maeneo tengefu ya Hifadhi za Wanyama na mapori ya akiba.
Amesema mkoa unaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kutekeleza maagizo hayo kwa lengo la kuwaondolea wananchi kero hiyo.
Aidha amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu kwa jitihada zake za kukabiliana na changamoto za wananchi kwa lengo la kuwaletea maendeleo.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa