WAZIRI MPINA AAHIDI KUPAMBANA NA UVUVI HARAMU NCHINI
Posted on: October 27th, 2017
Kiamakikubwa kwa, wavuvi harama na waingizaji wa zana za uvuvi harama inakuja, Mhe. Waziri Luhaga Mpina ameyasema haya wakati wa Ziara yake ya kikazi Mkoani Kigoma mara baada ya kupokea taarifa ya Mkoa wa Kigoma kuhusu halialisi ya uvuvi katika ziwa Tanganyika.
Amesema aiwezekani vita ya uvuvi haramu inasemwa kila siku halafu haiishi “ hivi hii kama ni vita ni vita ya namna gani haina mwisho, mimi kama waziri mwenye zamana nasema siwezi kukubali nikishindwa nitajiondoa katika wadhifa huu”. Amesema Luhaga.
Ameeleza kabla ya hajajiondoa lazima wahusika wa uvuvi haramu na watendaji au mtu yeyote awaye mwenye kujihusisha na uvuvi haramu lazima amshughulikie ipasavyo. Hiwezekani serikali ipo, wataalam wapo na vyombo vya ulinzi vipo halafu tuendelee kuchezewa na watu wachache kwa maslai yao binafsi amesisitiza Mhe. waziri
Mbali na uvuvi haramu kuhatarisha upotevu wa mazalia ya viumbe vya majini, pia umekuwa chanzo kikubwa cha uhatarishi wa afya zetu, magonjwa ya kansa na moyo yanaongezeka kutokana na utumiaji wa sumu, baruti na mabomu kuvua vitoeo vya majini
Kwa kipindi cha mwaka 2016/2017 jumla ya Zana haramu zenye kukadiriwa kuwa na thamani ya Shillingi za Kitanzania 480,675,000 ziliteketezwa Mkoani Kigoma ambazo zilikamatwa mwambao wa Ziwa Tanganyika.
Zana hizo Kokoro 66, monofilament/timber 173, vyandarua (kokoro) 45, makila ya undersize 47, mitimbo 3, maboksi ya kuhifadhia samaki 8, Kamba Mita 22,500 na samaki wachanga zaidi ya kilo 720.
Mhe. Mkuu wa Mkoa amesisitiza kuwa serikali ya Mkoa itaedelea kulinda rasilimali za Ziwa Tanganyika kwa kusimamia uvuvi edelevu kwa vizazi vijavyo, amewatahhadharisha wavuvi na wanannchi kuepukana na vitenndo vya uvuvi haramu, ikumbukwe kuwa wavuvi wa zana zote wanapaswa kuzingatia Sheria na kanuni zilizowekwa ili kuhifadhi rasilimali ya uvuvi iwe endelevu na yenye manufaa kwa jamii nzima.