Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amewasili mkoani Kigoma ambapo kesho Mei 6,2024 atashiriki na kufunga kikao cha pamoja cha wataalam wanaoziwakilisha nchi za Tanzania na Burundi kinachofanyika mkoani hapa kwa lengo la kujadili urejeaji wa wakimbizi wa Burundi.
Akitoa taarifa ya maendeleo ya Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye, amesema hali ni shwari, ni msimu wa mavuno ambapo hali ya chakula ni toshelevu sambamba na serikali kuendelea kuimarisha miundombinu mbalimbali kwa ajili ya kuboresha huduma mbalimbali za kijamii.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa