Mkuu wa mkoa ameyasema hayo wakati alipokutana na kuzungumza na makundi maalumu ya wazee na watu wenye uelemavu wa Mkoa wa Kigoma.
Mkuu wa Mkoa amewaomba watu ulemavu na wazee kukemea tabia za baadhi ya watu ambao wanaingia mitaani na kuwa ombaomba badala ya kujihangaisha kufanya kazi kwa kisingizio cha uelmavu na uzee.
“Tumieni fursa ya kuomba mikopo lakini mjitahidi kukopa kwa malengo kwani Serikali ya awamu ya tano chini ya Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia imeweka utaratibu mzuri wa kuwawezesha makundi maalumu wa kuwakopesha walemavu kuptia asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri; na sasa imeruhusu mikopo ya mtu mmoja mmoja tofauti na awali ambapo ilikuwa hadi watu waunde kikundi”
Halmashauri kuzingatia maelekezo na maagizo ya Serikali ya kutoa asilimia 2 ya makusanyo ya ndani kwa watu wenye ulemavu,vijana na akinamama. Amesema sharia ya mikopo imeshabadirishwa kutoka kukopeshwa kikundi hadi kukopeshwa mtu mmoja mmoja mwenye sifa, “sitegemei kwamba kutakuwa na kisingizio kuwa hawana vikundi, ni wasumbufu, hawarejeshi a sababu nyinginezo zenye nia ya kukwepa Majukumu” alisama Andengeye.
Aliongeza kuwa Serikali ya Mkoa itafuatilia kujua kila Halmashauri ilipaswa kukopesha kiasi gani na wamekopesha asilimia ngapi kwa Watu Wenyee Ulemavu tofauti na hapo lazima wahusika waanze kuwajibishwa.
Kwa upande wa wataalamu Maafisa maendeleo ya jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii amewataka kutoka ofisini na badala yake kwenda kuwatembelea makundi maalumu kujua changamoto zao na kuzitafutia majawabu. “pale inapoonekana hawakidhi vigezo vya mikopo kwa upande wa watu wenye ulemavu ninyi maafisa ni jukumu lenu kuona namna ya kuwasaidia ili wapate vigezo kama ni kuwashauri bishara za ili kujipatia kipato na kumudu maisha yao” alisisitiza
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa