Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma imepongezwa kwa hatua ya kutekeleza zoezi la kuwatambua na kuwapatia kadi za matibabu bure wazee wenye umri kuanzia miaka 60 na wasio na uwezowa kuigharimia matibabu .
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brig. Emanuel Maganga wakati wa kukabidhi kadi za matibabu bure kwa wazee kutoka katika kata 20 Wilayani Buhigwe, zoezi la ugawaji vitambulisho vya msamaha wa matibabu kwa wazee wasio jiweza ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wazee Duniani, ambayo huazimishwa kila tarehe mosi Oktoba.
Niwapongeze uongozi wa Wilaya ya Buhigwe kwa kutekeleza agizo la serikali ambalo lipo kisheria na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015, ninamini vitambulisho vya msamaha wa matibabu wazee wasio jiweza vitawaondolea usumbufu waliokuwa wanapata wanapohitaji matibabu.
Maganga amezitaka Halmashauri zote Mkoani Kigoma, kuhakikisha hadi mwisho wa mwaka 2018 ziwe zimeshafanya utambuzi wa wa Wazee kuwa na kanzi data na kuwagawia kadi za msamaha wa matibabu.
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Buhihwe Bw. Anosta Nyamogaalisema Wilaya ya Buhigwe katika mwaka 2017/2018 jumla ya wazee 14,993 walitambuliwa katika kata 20 zilizopo. Aidha, kati ya hao Wazee 11,152 sawa na asilimia 74 ya wazee wote ni hawajiwezi kiuchumi.
Ameongeza kuwa kwa kuanzia Halmashauri imeanza kwa kugawa kadi 10,050 kati ya 11,152 sawa na asilimia 9 ya utekelezaji katika awamu ya kwanza inayohusisha kata 10 , "zoezi hili ni endelevu kama sera na miongozo zinavyoelekeza
Kwa upande wao wawkilishi wa Wazee Wilayani Buhigwe wameishukuru Serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kutambua kwamba wazee ni rasilimali na hazina kubwa katika maendeleo ya nchi.
Wazee hao wameiomba Serikali kuendelea kuzishughulikia changamoyo mbalimbali zinazowakabili katika jamii ikiwa ni pamoja na Sera ya wazee ya mwaka 2003 kuto fahamika na kutekelezwa, wazee kudharauliwa na kuto heshimiwa, kufanyiwa ukatili, kudhurumiwa mali, na matunzo duni.
Aidha, wameeleza bado utaratibu wa kutoa huduma bure kwa wazee una mapungufu, kutoshirikishwa katika vyombo vya maamuzi, kutozingatiwa haki za wazee, uhaba wa wataalamu wa masuala ya wazee mfano maafisa Ustawi jamii.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa