m
MKUU WA MKOA WA KIGOMA THOBIAS ANDENGENYE AKIZUNGUMZA NA WAJUMBE WA KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA KIGOMA (HAWAPO PICHANI) KILICHOFANYIKA JULAI 20, 2023 KATIKA UKUMBI WA NSSF MANISPAA YA KIGOMA UJIJI.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye ameongoza kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa Leo Julai 20, 2023 kilichofanyika katika Ukumbi wa NSSF Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Kupitia kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wamewataka wakazi mkoani hapa kuheshimu mipaka ya maeneo Tengefu ya Hifadhi za Barabara kwa kutofanya shughuli za kibinaadamu katika Maeneo hayo.
‘’Kupitia Kikao hiki, nawaagiza Wakuu wa Wilaya, TANROADS pamoja na TARURA kuhakikisha hakuna Mwananchi anayejenga kwa ajili ya Makazi au Shughuli zozote za kibiashara’’ ameagiza.
Amefafanua kuwa, kuwaacha wananchi hao wakifanya Shughuli za kibinaadamu katika maeneo hayo kunachangia kusababisha Fidia na Madai yasiyokuwa ya Lazima Serikalini wanapotakiwa kupisha katika maeneo hayo katika Siku zijazo pia ni hatari kwa usalama wao.
‘’nitoe wito kwa wananchi wanaoendelea kuzitumia hifadhi hizo za Barabara kwa shughuli zao kuondoka kwa hiyari badala ya kusubiri kulazimishwa kufanya hivyo na mamlaka za kiserikali’’ amesisitiza Mkuu wa Mkoa.
Katika Hatua nyingine, Andengenye amewaagiza Viongozi wa TANROADS na TARURA kutosita kuwachukulia Hatua wakandarasi wazembe watakaoshindwa kukamilisha Miradi wanayoitekeleza kwa wakati.
Katika hatua nyingine, Kiongozi huyo wa Mkoa ameisisitiza Mamlaka za Barabara vijijini na Mijini(TARURA) kuongeza kasi katika kupanua mitandao ya Barabara maeneo ya vijijini kutokana na Shughuli nyingi za uzalishaji kufannyika katika Maeneo hayo.
Naye Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Mkoani hapa(Kisez) Deogratius Sangu, amezitaka Mamlaka hizo zinazohusika na Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara kuweka mpango wa Ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha Lami kuelekea lilipo eneo hilo ili kuendelea kuwavutia wawekezaji.
KATIBU TAWALA MKOA WA KIGOMA ALBERT MSOVELA, AKIZUNGUMZA NA WAJUMBE WA KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA KIGOMA.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa