Watumishi wa Idara ya Elimu wametakiwa kutumia fursa ya mafunzo yanayotolewa na wadau wa Sekta hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo kwa kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na kuleta matokeo chanya kielimu mkoani hapa.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Kigoma Hamimu Tambwe wakati akifungua mafunzo kwa Wataaluma na Maafisa Elimu Msingi, Wathibiti Ubora wa Elimu pamoja na Makatibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu ngazi ya Mkoa, yaliyolenga kuwajengea uelewa kuhusu Hadithi za Mafanikio ya Kujifunza ili kuboresha zoezi la ufundishaji na ujifunzaji.
‘‘Wadau wa Elimu wanafadhili miradi mbalimbali ya kielimu kwa lengo la kuinua ubora wa elimu yetu hivyo tunapaswa tuutumie ufadhili na misaada hiyo katikakuoresha kiwango chetu cha elimu’’ amesema Tambwe.
Mratibu msaidizi wa Mradi wa Shule Bora (TAMISEMI)Bi. Adelaida Pangani, amesema mafunzo hayo yanatolewa kwa viongozi hao wa kitaaluma kwa lengo la kuwajengea uelewa ili waweze kufuatilia maendeleo ya utekelezaji kwa watendaji wa Darasani ambao ni Walimu wakuu, walimu wa taaluma pamoja na walimu mahiri.
‘‘Tunawajengea uwezo wakuu wa Idara na vitengo vya kielimu ili wakati wa utekelezaji wa mradi huu shuleni kuwepo na usimamizi mzuri pamoja na ushirikiano baina ya watendaji na wasimamizi’’ amesema Bi. Adelaida.
Mafunzo hayo yamelenga kuimarisha mbinu za ufundishaji na ujifunzaji ili kuboresha Taaluma mkoani Kigoma na maeneo mengine ambayo mradi wa Shule Bora unatekelezwa.
Hadithi za Mafanikio za kujifunza za mfano ni hadithi thibitisho ambazo huelezea mabadiliko chanya kuonesha jinsi mabadiliko hayo yanavyomnufaisha mjifunzaji. Pia huboresha tija na ufanisi katika ufundishaji wa Mwalimu
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa