Viongozi na Watendaji katika Halmashauri zote Mkoani Kigoma wametakiwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea ya kukaa ofisini, kusumbua wananchi wanapowafuata kuhitaji huduma
katika ofisi zao na wale wanaoendelea na vitendo vya rushwa kuacha mara moja.
Kaulio hii imetolewa na Mkuu wa Mko wa Kigoma Mhe. Brig.Jen. (Mst.) Emmanuel Maganga baada ya kukamilisha zoezi la kuwasikiliza wananchi mbambali wenye kero na
malalamiko katika Wilaya ya Kasulu.
Mhe. Maganga amejipangia siku ya kusikiliza kero na malalamiko mbalimbali ya wananchi siku ya jumatano kila wiki ambapo kila Wilaya hutembelewa na wananchi kuwasilisha
kero na malalamiko
Maganga amesema kuwa kero nyingi alizosikiliza kati ya wananchi 61 zaidi ya 85 asilimia ni malalamiko ya mogogoro ya Ardhi ambayo imesababishwa hasa na watendaji wa
Idara ya ardhi kufanya kazi kwa mazoea pamoja na viongozi kutosimamia vizuri maeneo yao.Migogoro mingine ambayo amesema inaweza kutatuliwa na watengaji pamoja na
viongozi ngazi ya Wilaya ni masuala ya mirathi.
Aidha amewataka wananchi kufuata sheria na taratibu za Kimahaka kwani kumekuwepo na wananchi wanaposhindwa katika ngazi kuu za Mahaka hawafuati taratibu na hivyo
kuanza kukimbilia kwa viongozi kinyume na taratibu za Kimahakama.
Naye Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kasulu ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe amemwahidi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kuyafanyia kazi malalamiko yote na kuyapatia suhluhu
amabyo yameelekezwa katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ndani ya Wiki moja.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255738192977
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa