WATENDAJI NA MADIWANI WATAKIWA KUZINGATIA MIPANGO YA UENDELEZWAJI MIJI
Posted on: October 23rd, 2017
Madiwani na watendaji katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wametakiwa kutimiza na kuzingatia masula ya kitaalamu ya Mpango Mkakati wa maendeleo wa Mji wa Kigoma Ujiji, kwa kuzingatia sheria, ufanisi na kutopindisha mipango jambo linalosababisha migogoro isiyo ya lazima.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali (mst.) Emmanuel Maganga wakati wa Mkutano Mkuu wa wadau wa Mji wa Kigoma Ujiji wa Mpango Kabambe wa Maendeleo ya Manispaa hiyo.
Maganga Amesema mpango huu siyo wa kisiasa bali unalenga kuleta tija kwa wakaI wa Mji wa Kigoma Ujiji hivyo tunapaswa kuutekeleza kwa ufanisi mkubwa. Tuwasaidie wananchi kuondoa kero za migogoro ya ardhi.
Ameongeza kuwa watendaji wa serikali kwa miaka iliyopita wamesababisha migogoro mingi ya ardhi kutokana na kutokuzingatia taratibu na sheria, kufanya kazi kwa kukuika mipango kazi ya maendeleo ya Mjiji iliyokuwepo hapo awali.
Aidha upande wa wananchi Brigedia Maganga amewataka waachenkuuziana nankununua mawneo bila kufuata taratibu za ardhi jambo ambalo linaweza kuwaingizia hasara za kutapeliwa ama kubomolewa majengo yao na serikali." Kuwa na fedha himaniniishinunawezankujenga popote bila kufuata utaratibu nawaomba wananchi wa Kigoma mlielewe hili" aliongeza Maganga.
Nao wadau mnalimbali walooshiriki katika mkutano huo wametoa maonia yao kwa kusisitiza elimu ya uelewa juu ya masuala ya ardhi inahitajika, kwani bila uelewa wa wananchi bado tatizo la migogoro ya Ardhi litaendelea kuwepo. Wananchi wanatakiwa kuelimishwa hatua zote za upatikanaji wa ardhi namna ya kuuza/kununua ili kuepuka watu zaidi ya mmoja kununua kiwanja kimoja au kununua maeneo ya wazi.
Mpango wa maendeleo wa Mji wa Kigoma Ujiji 2017-2037 umelenga kuboresha Mji kwa kuondoa tatizo la ukuaji wa mji, ujenzi holela na uvamizi wa maeneo ya uwekezaji na yale ya wazi. Aidha mpango huu utaugharisha mji wa kigoma ambao unatajwa kuwa ni Mji wa Kimkakati kutokana na fursa mbalimbali za kibiashara, kilimo, na viwanda ambapo katika Nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Zambia, Mji wa Kigoma ndiyo Lango kuu katika nyanja mbalimbali kiuchumi.