Wanufaika wa Mikopo katika Halmshauri watakiwa kuitumia vizuri.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brig.Jen. Emmanuel Maganga amewataka wanufaika wa Mikopo inayotolewa na Halmashauri kuhakikisha wanatumia mikopo hiyo kwa kutekeleza malengo waliyojiwekea na kufanya marejesho kwa wakati ili vikundi vingine viweze kunufaika.
Mhe. Maganga amesema hayo wakati akikabidhi hundi ya mkopo ya Shilingi Milioni 85 kwa vikundi vya wanawake, Vijana na Walemavu zilizotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza.
Ninawaomba mikopo hii mnayopata kwenda kuitumia kwa malengo ya kikundi mliyojiwekea. Kumekuwwepo na tabia ya baadhi ya vikundi wanapopewa mikopo hii hubadiri mawazo na malengo ya kikundi na kuamua kuzigawana fedha kwa matumizi binafsi,kumbukebi fedha hii haina riba, Serikali imeamua kuweka sheria hii ya Halmshauri kutoa asilimia 10 ya makusanyo ya mapato ya ndani ya kila mwezi ili kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi, na njia nzuri ya ilionekana kupitia vikundi na siyo mtu mmoja mmoja.amesisitiza Maganga.
Akitoa taarifa ya utoaji wa mikopo katika Wilaya ya Uvinza Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mhe. Mwanamvua Mrindoko amemweleza Mkuu wa Mkoa kuwa hadi sasa Halmahsuri meshatoa shilingi milioni 92.1 tangu mwaka wa fedha uanze sawa na asilimia 98 ya lengo la Mwaka.
Aidha, Mhe. Mrindoko amewasisitiza Vijana, akinamana na Walemavu kujiunga kwenye vikundi na kutengeneza malengo yao ya kiuchumi ili waweze kukopeshwa kwani ni haki yao kupata mikopo hiyo.
utoaji wa mikopo hii ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama ha Mapinduzi ya Mwaka 2015 Ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanawezeshwa kiuchumi, Serikali inatoa mikopo ya asilimia 10 zinazotokana na mapato ya ndani ya halmashauri ambapo mipango yote ya uwezeshaji kiuchumi inawajumuisha pia vijana, Kinamama na watu wenye ulemavu
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa