WARUNDI WANYAKUA KOMBE FAINALI ZA LIGI YA UJIRANI MWEMA KIGOMA
Posted on: October 28th, 2017
Michezo ya mchuanoa ya ujirani mwema ya Ligi ya Lake Tanganyika Cup imemalizika kwa timu ya Mwamgongo ya Mkoani Kigoma kufungwa na timu ya black eagle kutoka Burundi 1-0.
Mbali na kuweka kizingiti kwa timu zote mbili, dakika za nyongeza zilibadili upepo na kuipa black eagle ushindi ambapo imejinyakuulia kombe pamoja na shilingi million 2.5, huku mshindi kwa pili mwamgongo akiondoka na milioni 2.
Nayo timu ya kasulu kambaini ilijinyakulia kitita cha mshindi wa tatu shilingi milioni 1.5 kwa kuizaba timu ya kakonko bao 2-1 hivyo kuwa mshindi wan ne nakujipatia shilingi milioni 1.