Wanaume Wahamasishwa kupima VVU
Mkuu wa Mkoa Mhe. Brig. Jen. (Mst.) Emmanuel Maganga ametoa wito kwa watu Mkoani Kigoma hususan wanaume, kujitokeza kwa wingi kupima VVU na kufahamu hali zao ili wanapogundulika na VVU waweze kuanza kutumia dawa za kufubaza VVU mara wanapogundulika na maambukizo.
Maganga ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa kampeni iliyozinduliwa kimkoa Wilayani Uvinza katika Tarafa ya Nguruka ya kuhamasisha wananchi hususan wanaume kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema. Amewasihi wanaume kuacha tabia ya kumsindikiza mama akipima yeye pekee nasi tunadhani tupo sawa.
Akielezea madhumuni ya kampeni hiyo kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Hosea amesema Kamapeni hiyo ya kitaifa yenye kauli mbiu“Furaha Yangu – Pima, Jitambue, Ishi”. Inaweka mkazo na kuhamasisha zaidi Wanaume kupima ili kutambua hali zao za maambukizo ya VVU. Hivyo, mpango huu una lengo la kumwanzishia dawa za ARV kila mtu aliye na maambukizo ya VVU ili aweze kuishi maisha ya furaha bila kuwa na hofu ya kupata magonjwa nyemelezi.
Aidha amazitaka Halmashauri Mkoani humo kwa kushirikiana na wadau wa mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI kufanya kampeni ya upimaji kwa wanaume mfululizo ili hadi mwezi Desemba mwaka huu 2018 wakati wa Maadhimisho ya siku ya UKIMWI, kuweza kupata halihalisi ya maambukizi katika Mkoa wa Kigoma.
“Wakuu wa Wilaya kwa kusaidiana na Wakurugenzi wa Halmashauri simamieni kampeni hii kwa uzito unaostahili, pia anzisheni mpango wa kuendesha upimaji kila panapokuwepo mikusanyiko katika Wilaya zenu” amesisitiza Mkuu wa Mkoa.
Ili kuendelea kupambana na maambukizi Mkoani Kigoma Halmashauri na Idara ya Afya zimeshauriwa kuhakikisha zinawatumia vyema Watu wanaoishi na VVU (WAVIU), hasa waliojiweka wazi hali zao, kuwahamasisha watu wanaorudi nyuma katika matumizi ya dawa za kufubaza (ARV). Nchini Tanzania
Hamasa miongoni mwa wananchi na hasa wanaume katika kuziendea huduma za upimaji wa VVU nchini bado ni ya kiwango cha chini Matokeo ya awali ya Utafiti uliofanyika katika ngazi ya kaya kuanzia mwezi Oktoba 2016 hadi Agosti 2017, yanaonesha ni asilimia 52.2 tu ya wanaoishi na VVU wenye umri wa miaka 15 – 64 walitoa taarifa kuwa wanajua hali zao za maambukizo ya VVU, (Wanawake ni asilimia 55.9 na Wanaume ni asilimia 45.3) WAVIU wa umri wa miakan 15-64 walitoa taarifa ya hali zao.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa