Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amemtaka Meneja wa Mamlaka ya Maji Mkoani Kigoma kuhakikisha wananchi wa Kijiji cha Kigembe wanapata maji ifikapo tarehe mosi Julai 2022.
Akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na fedha za mpango wa maendeleo UVIKO 19 amesema Serikali ya Mama Samia inayo dhamira kubwa ya kuhakokisha wananchibwanapata huduma za kijamii karibu yao.
Amwsema kinachotakiwa kwa watendaji ni kuahikisha huduma zonapatikana na siyo kutoa maelezo mengi na mipqngo ya kwenye karatasi ambayo haiwasaidii wananchi"wananchi hawa wanahitaji kuyaona maji yakitoka katika mabomba na siyo vinginevyo" alisisitiza Andengenye
Nao wananchi wameelezwa kufurahishwa na kasi ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Samia Suluhu Hassan kwa kasi kubwa anayoendelea nayo ya kuwaletea miradi mingi ya maenseleo ambayo inagusa moja kwa moja maisha yao.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa