Wananchi wa Kijiji cha Nyamidaho Tarafa ya Makere Wilayani Kasulu Wameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuwajengea kituo cha Afya cha Kisasa kitakachohudumia takribani watu 176212 wa Tarafa ya Makere .
Wananchi wameelezea kufurahishwa na hatua ya Serikali ya awamu ya tano kwa kutenga fedha kwaajli ya kuboresha Afya katika. Wakisoma risala yao mbele ya Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brig. Jen. Mst. Emanuel Maganga wamesema awafikishie Salam zao za upendo kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli.
Akiweka jiwe la Msingi katika Kituo cha Afya Nyamidaho Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brig. Jen. (Mst.) Emanuel Maganga amewasifu wananchi kwa kushirikiana na Serikali katika kutekeleza ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya Kituo cha Afya cha Nyamidaho.
Katika Taarifa iliyosomwana Mkurugeni wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Vijijini Mhandisi Godfrey Kasekenya imeeleza kuwa serikali kuu ilitoa Tshs milioni 500 kwaajili ya ukarabati wa kituo hicho cha afya,lakini kwa kutumia Force Account wamefanikiwa kujenga Jengo la Wagonjwa wa nje OPD ambapo mchangonwa nguvu za wananch ulikuwa 37,800,00
Jumla ya Tshs 537,800,000 zimetumika katika Ukarabati wa Kituo cha Afya cha Nyamidaho pamoja na Ujenzi wa majengo sita ikiwemo Wodi ya akinamama Wajawazito na watoto wachanga, jengo la kuhifadhia maiti, maabara, jengo la Upasuaji pamoja na wagonjwa wa nje. Aidha miundombinu mingine iliyojengwa ni nyumba ya Mganga, pia ukarabati wa nyumba za watumishi nanmiundombinu ya maji.
Aidha Mhe. Mkuu wa Mkoa amewa kuwakumbusha na kuwahimiza wananchi kujiunga na Bima ya Afya ili waweze sasa kufaidi uwepo wa kituo cha afya katika karibu yao. "Wananchi jiungeni na mfuko wa Bima ya Afya ili kuokoa gharama za matibabu. CHF iliyoboreshwa imeweka utaratibu mzuri wa matibabu ambapo sasa inaruhusu mfumo wa rufaa kutoka ngazi za chini za kutolea huduma hadi ngazi ya Mkoa tofauti na utaratibu wa zamani uliowezesha mgonjwa kupata huduma kwenye kituo kimoja kilicho karibu na mgonjwa, bali itawasaidia sana katika kupata huduma za afya kwa gharama nafuu" amesisitiza Mhe. Mkuu wa Mkoa.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa