Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Kigoma wamekumbushwa kumuenzi Baba wa Taifa hayati Julius Kambarage Nyerere kwa kutenda yale aliyoyaishi enzi za uhai wake.
Haya yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brig. Jen. (Mst) Emmanuel Maganga aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa kupokea msafara wa Matembezi ya hiari ya Wananchama wa CCM Mkoani Kigoma yenye lengo kumuenzi Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere.
Akihutubia wananchama hao Mkuu wa Mkoa Maganga amewakumbusha mambo mbalimbali ambayo hayati Baba wa Taifa aliyapenda na ambayo aliyachukia “Niwakumbushe tu mambo machache ambayo na sisi kama wanachama na Viongozi tunapaswa kuyaishi ili kumuenzi Baba wa Taifa”.
Mwl. Alikuwa mzalendo wa kweli na alisisitiza Uzalendo kwa watanzania, tudumishe uzalendo kwa Nchi yetu.
Katika kuwatumikia wananchi mwl. Alisisitiza sana uadilifu kwa Viongozi katika kuwatumikia wananchi
Mwl.alipenda kila mtu awe huru kutoka katika utumwa ndiyo maana alipigania Uhuru wa Tanganyika, hata nchi nyingine za kusini mwa Afrika alitumia rasilimali za nchi ili tu kuwasaidia wawe huru, hakupendezwa na manyanyaso ya aina yoyote. Alisisitiza sana Kujitegemea kuwa Uhuru Kiuchumi na Kisiasa
Mwl alipenda umoja, na ili kujenga umoja wetu alisisitiza Lugha ya Kiswahili kitumike kuwaunganisha watanzania wote, kuleta mshikamano na kudumisha Amani katika jamii ya watanzania.
Mwl. Aliichukia rushwa na kuipiga vita vikali, hakuwa Rafiki wa watu wenye uchu wa mali na madaraka, kwani alijua kabisa vyote hivyo ni kinyume cha haki za mwanadamu na huvuruga demeokrasia. Katika maisha haya tumuenzi Baba yetu wa Taifa kwa vitendo ndipo tutakuwatumempa heshma, amemalizia Mkuu wa Mkoa.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa