Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kuanza mchakato wa kumalizia uhakiki, uandikishaji na utambuzi wa nia ya wakimbizi kutoka Burundi wanaoishi katika vijiji mbalimbali Mkoani Kigoma, ambao waliandikishwa mwaka 2010.
Jumla ya wakimbizi 22,477 kutoka Burundi walisajiliwa mwaka 2010 ikiwa ni hatua ya kuwatambua na kuanza mchakato wa kutafta suluhisho la kudumu la wakimbizi hao wenye takribani miaka 35 wakiwa wanaishi Moani Kigoma na maeneo mengine nchini Tanzania Tanzania.
Akizungumza wakati wa kufungua warsha ya mafunzo kwa maaafisa na viongozi kutoka ngazi mbalimbali serikalini na shirika la kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emanuel Maganga amesema zoezi litawahusu wakimbizi wa kutoka Burundi Burundi wenye asili ya vijiji vya Mkoa wa Kigoma na wanaoishi Ndani na nje ya Mkoa wasio na Suluhisho la Kudumu juu ya ukimbizi wao Nchini Tanzania.
Amesema zoezi hili litasaidia kupata tarifa zao kamili na kusaidia kupata maamuzi ya msingi ya mchakato wa kutafuta suluhuisho la kudumu kwa kundi la wakimbizi wa mwaka 1972.
Naye Mkurugenzi msaidizi kutoka Wizara ya mambo ya Ndani Idara ya Wakimbizi Suleiman Mziray amesema zoezi hili huenda likawa ni fursa ya mwisho kutolewa na serikali ya Tanzania kwa wakimbizi wa mwaka 1972 kutoka Burundi wenye asili ya vijiji vya Mkoa wa Kigoma nchini Tanzania, ambao hawajapata suluhisho la kudumu.
Zoezi kama hili lilifanyika mwaka 2007 ambapo wakimbizi wapatao 162156 walipatiwa urai wa Tanzania na wakimbizi takribani 53000 walirudishwa kwa hiari katika nchi yao ya asili.
Mnamo 1972, Tanzania ilipokea maelfu ya wakimbizi kutoka Burundi na ndani ya nchi iliwaweka katika makazi matatu ya Katumba, Mishamo na Ulyankulu inayojulikana kama Makazi ya Kale. Miji miwili Katumba na Mishamo ni katika Mkoa wa Katavi wakati Ulyankulu iko katika Mkoa wa Tabora. Wengine wakimbizi kutoka kesi hiyo hiyo walikuwa wamewekwa katika vijiji vya Mkoa wa Kigoma. Baadaye, baadhi ya wakimbizi kutoka miji yote na Kigoma walihamia kuishi mahali pengine nchini Tanzania.
Serikali ya Tanzania, kwa kushirikiana na UNHCR ilifanya sensa ya idadi ya wakimbizi wa 1972 kati ya Julai na Septemba 2007 ambapo baadhi ya wakimbizi 218,234 wa Burundi wa mwaka 1972 waliandikishwa. Wakati wa usajili, wakimbizi waliulizwa kuhusu suluhisho ambalo walipendelea kati ya kurudi kwa hiari na asili na ushirikiano wa kudumu nchini Tanzania.
Matokeo ya usajili yalionyesha kuwa asilimia 20 ya wakimbizi walipenda kurudia Burundi wakati wengine 80% walipendelea kuomba asili kama Watanzania.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa