Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brig. Jen. (Mst) Emmanuel Maganga amewataka wananchi wa Mkoa wa Kigoma kuchangamkia fursa mbalimbali ambazo zimekuwa zikiletwa Mkoani humo na Mashirika mbalimbali ya maendeleo kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.
Maganga amesema kuna mashirika na miradhi mbalimbali ambayo inafedha na inataka watu binafsi, vikundi, wafanyabiashara kuchangamkia fedha zinazotolewa kwa mikopo nafuu au kama ruzuku ili waweze kuwekeza na kukuza mitaji yao.
Akikagua miradi ya inayofadhiliwa na Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara amesema mradi huo upo kwaajili ya kutengeneza mazingira mazuri na kuwasaidia wananchi katika sekta ya kibiashara, kuwawezesha kwa mitaji na, vifaa na pamoja na miundombinu hivyo ni nafasi nzuri kwao kuchangamkia fursa hiyo.
Mradi wa Kuimarisha Mazingira ya Uwekezaji wa Ndani umeonekana kuwasaidia wafanyabiashara na wawekezaji kwa kuwapatia mashine na kuwajengea miundombinu mbalimbali ili kukuza na kuboresha biashara na mitaji yao.
Naye Anselmo Matabaro Kaimu Katibu wa TCIAA Wilaya ya Kibondo, ametoa shukrani kwa mradi huo na uongozi wa Wilaya ya Kibondo kwa kuendelea kushirikiana na sekta binafsi katika hatua mbalimbali kuboresha mazingira ya kiabiashara Wilayani Kakonko.
Hadi sasa mradi wa LIC umewanufaisha wananchi mbalimbali kibiashara. Smabamba na kununua wa mashine za kukusanyia mapato za Halmashauri ili kuongeza mapato. Lengo kuweka mazingira wezeshi ya kibiashara na wafanya biashara. Kujenga vituo vya kibiashara katika Halmashauri zitakazowezesha wafanyabiashara kupata taarifa na huduma mbalimbali za kibiashara katika sehemu moja.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa