Wakala wa Majengo Tanzania TBA wameonywa kuwa na tabia za ucheleweshaji wa kumaliza miradi mbambali wanayopewa na Serikali jambo ambalo linakwamisha utoaji wa huduma katika miradi hiyo kama ilivyokusudiwa.
Serikali ilitoa fedha kwaajili ya ukarabati wa miundombinu kwa shule na vyuo vya zamani ambazo majengo yake na miundombinu ilikuwa imeshaakaa, kwa Mkoa wa Kigoma shule 16 ikiwemo Shule ya Sekondari ya Kigoam iliweza kupatiwa shilingi milioni 900, ambapo Mkandarasi Wakala wa Majengo Mkoani alipatiwa kazi hiyo.
Hata hivyo kumekuwa na kasi ndogo pamoja na utendaji usio wa kurishisha katika kufanya ukarabati wa miundombinu katika shule hiyo, kitendo ambacho kimefanya kuchelewa kukamilishwa kwa huduma muhimu kama vile vyoo, mabafu na mabweni.
Hadi kufikia muda wa wanafunzi kurudi kuanza muhula mwingine wa masomo mwaka 2018 bado wakala wa majengo Mkoani Kigoma walikuwa bado hawajakamilisha ukarabati wa miundo mbinu ikilinganishwa na fedha mabayo tayari imekwishakutolea awamu ya kwanza shilingi milioni 400.
Hali hii inamtia hasira si Waziri wa Elimu peke yake bali hata Mkuu wa MKoa wa Kigoma ambapo walipofanya ziara ya kukagua kazi zilizofanywa, ikaonekana ni mchezo wa kuigiza.
Akizungumza katika ziara ya kukagua ukarabati wa shule ya sekondari Kigoma Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako alimwambia Meneja Wakala wa Majengo Mkoani Kigoma kuacha ubabaishaji na kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano.
Inaonekana meneja hujui kazi yako, haiwezekani tangu mwezi Agosti 2017 mpaka leo hii hakuna kazi ya kuonekana uliyokwisha imaliza, wanafunzi wanasiku tatu wafungue bado vyoo havieleweki, unacheza na maisha ya binadamu, hili halikubaliki katika serikali ya awamu ya tano alisisitiza Prof. Ndalichako
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brig. Jen. Mstaafu Emmanuel Maganga ameshangazwa na kitendo cha wakala wa Majengo Mkoani Kigoma cha kushindwa kumaliza ukarabati wa Shule ya sekondari ya Kigoma pamoja na kuwa Serikali imeshatoa fedha karibu nusu ya gharama kwaajili ya ukarabati tangu Agosti, 2017.
Kufuatia hatua hiyo amabayo inaashiria uzembe, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma aliamuru kuwekwa mahabusu Meneja wa Wakala Mkoani Kigoma Bw. Mgalla Mashaka kwa uzembe wa usimamizi na kushindwa kutoa maelezo sahihi ya nini kilichokwamisha kutomalizika kwa ukarabati wa shule hiyo.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa