Serikali Mkoani Kigoma imewataka vijana na akinamama wakulima kujiunga katika vikundi ili waweze kukidhi vigezo vya kupata mikopo ambayo hutolewa na Halmashauri kupitia makusanyo ya ndani, ambapo kila Halmashhauri hutenga asilimia 10 ya makusanyo na kutoa mikopo kwa Vijana asilimia 5 na asilimia 5 kwa kinamama.
Haya yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali Emanuel Maganga (mstaafu) alipoweka jiwe la msingi katika mradi wa kuongeza thamani zao la Muhogo wa Kikundi cha KIADO.
Kwa miaka migi wakulima wa Mhogo Mkoani Kigoma wamekuwa wakiuza zao hilo kama mhogo ghafi jambo ambalo aliwapi tija kiuchumi. Zao la Mhogo hutumiwa kama Chakula na wakazi wa Mkoa wa Kigoma, Wakulima huuza kama zao ghafi, Wakulima wa zao la mhogo hutegemea soko lao katika nchi za Burundi, Rwanda, Uganda hadi Sudani kusini.
Mhe. Maganga aliwaeleza kuwa kuna haja ya vijana na kinamama kubadilika kutoka katika dhana ya ubinafsi kuelekea kujiuga katika vikudi ili kuweza kunufaika na mikopo ya fedha zinazotolewa na serikali. “mkijiuga katika vikudi mapata fursa ya kukopesheka na mnakuwa na uwezo wa kufanya kitu kikubwa chenye manufaa kuliko mtu mmoja mmoja, kupitia vikundi mnaweza kujenga viwanda vidogovidogo vitakavyofanyakazi ya kuchakata mazao” alisisitiza
Kujengwa kwa viwanda vidogovidogo kutatoa mwanya kwa vijana na kinamama kupata ajira katika shughuli za uchakataji, na kufugasha na hivyo kufikia adhma ya Serikali ya awamu ya tano Kuelekea nchi ya viwanda na Uchumi wa kati
Hivyo kuongeza thamani ya zao la mhogo kutakuza a kuonngeza patio la mkulima wa mhogo katika mkoa wa Kigoma tofauti na hapo awali, hii ni fursa kwa wakulima wa zao la muhogo na nikichocheo cha maendelo Kuelekea viwanda vikubwa kwanni dhana ya viwanda hata katika nchi zilizoendelea chimbuko la viwanda vikubwa linatokana na viwanda vidogo.