Serikali ya Mkoa wa Kigoma inatarjia kufanya operesheni ya kuwaondoa Wafugaji waliopo katika Pori la akiba la Kigosi Muyowosi lililopo Wilayani Kibondo ili kunusuru uhifadhi wa pori hilo pamoja na wanyama wanaopatikana humo.
Maamuzi haya yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma alipofanya kikao cha Kamati ya Ulinzi ya Wilaya ya Kibondo pamoja na Viongozi mbalimbali wa Wilaya za Kibondo, na Uvinza kikichoketi kuangalia namna ya kuanza operesheni ya kuondoa mifugo katika maeneo ya hifadhi.
Amesema Mkuu wa Mkoa Maganga kuwa hivi karibuni, Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utaliii alipofanya Ziara ya Kikazi Mkoani Kigoma mara baada ya kutembelea pori hilo alijionea uharibifu unaofnywa kutikana na uwepo wa mifugo mingiambapo liltolewa agizo wafugaji hao kuondoka mara moja ndani ya Siku saba.
Kimsingi wafugaji waliopo pori la Muyowosi wanapaswa kuondoka haraka wasingoje tuwaondoe kwani taarifa zinaonesha tangu mwaka 2003 wafugaji hao walilipwa fidia na kutafutiwa eneo la kwenda hata hivyo wachache waliendelea kubaki hadi leo kinyume na sheria, sisi tutaenda kuwaondoa, wale walioanza kuondoa nawpongeza kwa hatua hiyo ya kutii maagizo ya serikali. Amesisitiza Maganga.
Jumla ya wafugaji 44 wenyenkukadiriwa na mifugo zaidi ya elfu 30, wanafugwa katika pori la Kigosi -Muyowosi,mara kadhaa wamekuwa wakidai kuwa mazingira ya kuwaondosha mifugo hao ni magumu kutokana na eneo walilopo kuzungukwa na maji ya Mto Malagarasi, hivyo kuendelea kuathiri Ikolojia pamoja na Wanyama, vitalu vya uwindaji hivyo kupunguza mapato yanayotokana na uwindaji.
Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa amewahakikishia wafuaji kuwa kuondoka katika pori hilo ni lazima na hakuna kisingizio kwamba ng'ombe watazama kwanye maj, amesema haiwezekni tukiwaambia waondoke wanasingizia ng'ombe kuzama huku wanapeleka mifugo minadani, tunajua kunannja tatu wanazopitisha kwenda minadani na ndizo hizohizo tutazitumia kuwahamisha. Ameoneza Mkuu wa Mkoa.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa