Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Mhe. Hassan Rugwa ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotekeleza miradi ya Maendeleo mkoani Kigoma kuweka utaratibu wa kushirikisha walengwa ili kujua uhalisia wa mahitaji yao, jambo litakalosababisha miradi hiyo kuwa na tija na kuwaketea manufaa ya moja kwa moja wananchi.
Katibu Tawala ametoa kauli hiyo alipokutana na kuzungumza na Mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Serikali ya Ubelgiji (Enabel) linalotekeleza Mradi wa Wezesha Binti Mkoani hapa Bi. Denise Lapoutre na kusisitiza kuwa, mapendekezo na utekelezaji miradi unapaswa kuzingatia mahitaji halisi ya wananchi wanaolengwa na mradi husika.
Amesema kutekeleza mradi ni jambo moja na kuleta matokeo chanya ni jambo linguine, hivyo wasimamizi wa miradi hiyo wanapaswa kuhakikisha kila upande unahusika katika kufikiwa kwa malengo yaliyowekwa ili walengwa waweze kunufaika.
Amesema kila mradi unapoanza kutekelezwa lazima jamii husika ihusishwe kwa kila hatua hali itakayoibua utayari na kuifanya jamii hiyo kuwa sehemu ya mradi husika.
Tumeshuhudia maeneo mengi miradi inaanzishwa lakini inashindwa kufikia malengo yaliyokusdiwa kutokana na wakazi kutohusishwa, hivyo niwashauri kila hatua ikiwemo ubainifu wa walengwa, mahitaji na matarajio ya mradi’’ amesema Rugwa.
Mradi wa Wezesha Binti unatarajiwa kutekeleza ujenzi wa mabweni nane kwa shule chaguliwa katika kila halmashauri ya mkoa, matundu tisa ya vyoo vya wasichana pamoja na chumba cha kujihifadhi kwa ajili ya mabinti waliofikia rika balehe.
Kupitia mradi huo, jumla ya Shule za sekondari 25 zitafikiwa huku jumla ya wanafunzi wa kike na kiume 12,750 wenye changamoto za kupata kazi za staha na zenye ujuzi watafikiwa mkoani Kigoma.
Mradi wa wezesha binti pia unalenga kuhakikisha watoto walioacha masomo wanarejea shuleni, kuendelea kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kupitia ujenzi wa miundombinu, kutoa ujuzi kwa watoto walioacha shule, kuwawezesha ujuzi utakaosadida vijana kujiajiri, kushirikiana na serikali kuviwezesha vyuo.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa