Wadau wa biashara kati ya TCCIA Kigoma na Burundi BFCCI Wakutana Kujadili Masuala ya kibiashara
Posted on: May 29th, 2017
Wadau wa biashara kati ya TCCIA Kigoma na Burundi BFCCI leo wamekutaa Mkoani Kigoma kujadili mambo mbalimbali yanayoweza kuleta sura mpya na mabadiliko chanya katika biashara kati ya nchi hizo mbili.
Akizungumza katika hotuba yake ya Kufungua Mkutano huo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali (mst.) Emauel Magaga alisema Mkutano wa wafanyabiasara wa nchi zote mbili utawawezesha wote kwa pamoja kuweka malengo, na shabaha ya kutumia fursa za kibiashara na maendeleo katika nchi zao, sambamba na kupanua Malengo ya Maendeleo endelevu (MSDGs).
Juhudi hizi ni malengo ya kusaidia nchi hizi mbili katika kuelekea maendeleo endelevu, kwa kushughulikia vipimo vya maendeleo ya kiuchumi, kuwepo kwa ushirikiano mazingira endelevu ya kibiashara, na kuangalia vikwazo mbalimbali vinavyoweza kutatuliwa ili kutengeneza mazingira rafiki ya wafanyabiashara wa pande zote mbili.
Tanzania na Burundi zina uwezo wa kuzalisha bidhaa, pamoja na kutambua changamoto za kibiashara kwa pamoja, ili ziweze kushirikiana, katika ngazi ya kimataifa hazinabudi kutengeneza mikakati endelevu ya kibiashara.
Mkutano huu utatoa mwongozo wa Serikali, sekta binafsi, washirika wa maendeleo, asasi za kiraia na wasomi juu ya njia bora ya kutekeleza mipango ya kuweka yenye manufaa zaidi kwa wafanyabiashara wa Burundi na Tanzania.
Ili kuwa na mapinduzi ya kibiashara katika hali halisi itahitaji kujenga uhusiano na wadau mbalimbali, kushirikiana viongozi wa kisiasa na watoa maamuzi, viongozi wa serikali, wanasayansi, walimu na watafiti, vyombo vya habari, sekta binafsi, vyama vya kiraia, wananchi na kama jamii aliongeza Maganga.
Aidha, nguzo kuu za kuvutia katika biashara na kufikia mapinduzi ya kiuchumi ni utawala na uongozi, uwezo na rasilimali, kanuni na viwango, teknolojia na maendeleo ni lazima zizingatiwe katika kufika malego ayo.