MKUU WA MKOA WA KIGOMA KAMISHNA JENERALI MSTAAFU WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MHE. THOBIAS ANDENGENYE AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI WA MADHEHEBU YA DINI PAMOJA NA VYAMA VYA SIASA MKOA WA KIGOMA (HAWAPO PICHANI).
KATIBU TAWALA MKOA WA KIGOMA MHE. HASSAN RUGWA NI MIONGONI MWA MWAJUMBE WALIOHUDHURIA KIKAO HICHO CHA MKUU WA MKOA NA VIONGOZI WA MADHEHEBU YA DINI NA VYAMA VYA SIASA MKOA WA KIGOMA.
PICHA YA PAMOJA YA MKUU WA MKOA WA KIGOMA MHE. THOBIAS ANDENGENYE (MWENYE MIWANI KATIKATI) AKIWA NA VIONGOZI WA MADHEHEBU YA DINI NA VYAMA VYA SIASA MKOA WA KIGOMA
KIGOMA.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye amekutana na viongozi wa Madhehebu ya Dini pamoja na viongozi wa vyama vya Siasa Mkoa wa Kigoma kwa lengo la kuwashukuru viongozi hao kwa kushiriki katika kuhamasisha, kuelimisha na kuhimiza jamii kushiriki zoezi la uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 kwaamani na utulivu.
Akizungumza na viongozi hao katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Andengenye amesema viongozi hao wamekuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha zoezi hilo katika mkoa na kusisitiza jamii kutoa ushirikiano kwa viongozi waliochaguliwa bila kujali itikadi za vyama vyao ili waweze kusukuma mbele gurudumu la Maendeleo mkoani Kigoma.
Amewaelezea viongozi hao kuwa wametambua umuhimu wao katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa kufikisha jumbe kuhusu maendeleo na hatua mbalimbali zinazohusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa, jambo lililochangia idadi kubwa ya wananchi kujitokeza na kushiriki.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano na Amani Mkoa wa Kigoma Shekhe Hamis Kipemba, amesema viongozi wa madhehebu ya dini wapo tayari na wataendelea kushirikiana na uongozi wa serikali ya mkoa katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali sambamba na kuendelea kuhubiri Amani, umoja na mshikamano kwa wanakigoma na watanzania kwa ujumla.
Upande wake mjumbe wa kikao hicho Mch. Michaeli Kurwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Makanisa ya kipentekoste Mkoa wa Kigoma ameushukuru uongozi wa mkoa na wasimamizi wa uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa kuwashirikisha viongozi hao katika hatua zote kuanzia muhimu kuanzia mwanzo hadi kukamilika kwa zoezi hilo.
Yassin Bakari ambaye ni Mwenyekiti wa umoja wa vyama vya Siasa Mkoa wa Kigoma(TCD) amesema uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka 2024 umeisha kwa Amani na usalama na hakuna matukio yoyote yaliyojotokeza na kusababisha athari kwa mali na uhai wa wakazi.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa