Viongozi mbalimbali Mkoani Kigoma wametaka uwekwe msisitizo mkubwa kwa wakandarasi wanaojenga barabara ya Nyakanazi -Kabingo yenye urefu wa kilomita 54 na Kasulu - Kidahwe yenye urefu wa 63 kwani wanaenda polepole mno.
Viongozi hao wameyasema hayo mbele ya Naibu Waziri wa Mawasiliano na Ujenzi Mhe. Mhandisi Astatasha Justus Nditiye( Mb) katika Kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Kigoma.
Hii imetokana na taarifa aliyotoa Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Kigoma Mhandisi Narcis Choma ambaye amesema kasi ya Mkandarasi anayeshughulikia barabara ya Nyakanazi - kabingo Wilayani Kibondo yenye urefu 54km Kasi yake si ya kuridhisha kutokana na Mkandarasi huyo kuwa na vifaa vichache na vibovu. Hadi sasa ni aslimia 35tu ya kazi ndiyo imekamilika ambayo ni kuweka baadhi ya madaraja na kumwaga vifusi.
Kwa mujibu wa taarifa ya wakala wa Barabara Mkoani Kigoma, barabara hizo zilitakiwa zikamilike Mwaka huu mwezi Desemba lakini kutokana na changamoto kadhaa muda umeongezwa hadi mwezi mei mwakani 2018.
Aidha mkandarasi anayejenga barabara ya Kasulu – Kidahwe yenye urefu 63 km nayo inasuasua pamoja na Serikali kutoa fedha zote kwa Mkandarasi huyo.
Viongozi hao wametaka wakandarasi hao waongeze kasi ili kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano na agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye aliwataka wakandarasi na Wizara husika kuharakisha ukamilishaji wa barabara hizo muhimu kwa wakazi wa Mkoa wa Kigoma.
Mkoa wa Kigoma kwa miaka mingi umeteseka kutokana nankukosekana kwa miundombinu bora ya barabara yenye kuunganisha na Mikoa mingine.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa