Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt.Simon Chacha amewashauri viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe kuhakikisha wanaanza ujenzi wa Zahanati kwenye eneo la Nyamule ambalo halina mgogoro na linafaa kwa ujenzi ili kuharakisha huduma za afya kwa wananchi.
Akizungumza na viongozi wa Kata ya jana Mwenyekiti wa CCM kata ya Kajana, mwenyekiti wa kijiji, Mwenyekiti wa Kitongoji na wajumbe wengine wa kamati ya kijiji amesema wananchi wanahamu ya kupata huduma za afya karibu lakini wanakwamishwa na migogoro isiyo na tija.
Dkt Chacha ametoa ushauri huo kufuatia kuwepo kwa mvutano wa muda mrefu baina ya Uongozi wa Kijiji na kata ya Kajana kuhusu eneo la kujenga Zahanati Wilayani Buhigwe.
Aidha, amesisitiza kuwa Fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kutekeleza mradi huo zinatakiwa kutumika mapema kabla ya mwaka wa fedha kuisha ikiwa sambamba na mradi huo kuhakikisha unakamilika kwa viwango yaani thamani ya fedha.
Katika ziara hiyo Dkt.Simon Chacha ameambatana watendaji wa serikali akiwemo Afisa Afya wa Mkoa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe, Katibu Tawala wa Wilaya , Afisa Ardhi na Mwanasheria wa Halmashauri.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa