Viongozi wa dini wameaswa kutokujiingiza katika mabishano ya kisiasa pamoja na kuizodoa Serikali, bali watafute namna nzuri ya kukaa na kuishauri serikali kwa maelewano na mazungumzo kwa nia ya kujenga.
Haya yamesemwa na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa ibada ya kuwekwa wakfu kwa Maaskofu wanne na Askofu Mkuu msaidizi Mmoja wa Kanisa la Pentekoste motmoto Mkoani Kigoma.
Amesema Serikali ya awamu ya Tano ni sikivu na itapenda kuona viongozi wa dini wanahubiri neno la Mungu, kuleta Amani, umoja na mshikamano wa kitaifa badala ya kujiingiza kwenye siasa hivyo kuleta mgawanyiko ndani ya waamini na kuvuruga amani. Wakati wowote viongozi wa dini mnapoona kunashida maha waoneni viongozi zungumzeni nao kwa nia ya kujenga kuliko kutumika kisiasa ameongeza Mhe. Makam wa Rais
Kwa upande wao Viogozi wa dini wa Kanisa hilo wameipongeza Serlikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusimamia haki na misingi ya sheria kuhakikisha rasilimali za Nchi zinatumika kwa manufaa ya watanzania wote badala ya watu wachache.
Akisoma hotuba ya kusimikwa kwa Maaskofu mbele ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Askofu Mkuu wa Kanisa la Pendekoste Motomoto lilipo Mkoani Kigoma, Ezra Enock Mtamya amesema Serikali ya Awamu ya Tano inastahili pongezi kubwa kwa juhudi kubwa inazozifanya katika kuhakikisha rasilimali za nchi zinaleta manufaa kwa watanzania.
Akofu Mtamya ametaja moja ya mambo makubwa ya kujivunia katika Serikali ya awamu ya tano ni juhudi kubwa za kurudisha taswira ya Tanzania kimataifa mambao ilikuwa imeshapotea ni ununuzi wa Ndege ambazo kwa sasa zimerudisha hesma na kuitangaza tanzania hivyo kukuza uchumi na kuvutia bishara na utalii, ujenzi wa Reli ya kisasa pamoja na kuweka vipaumbele katika elimu na Afya.
Sisi kama viongozi wa dini tutaendele kuwaomba waumuni kuwaombea Viongozi wetu na serikali yetu ili iendelee kufanya mambo mazuri zaidi, alisisitiza Askofu Mtamya.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa