Umoja wa Vyama vya Siasa Mkoani Kigoma umeonesha kuridhishwa na namna ambavyo Serikali mkoani Kigoma ilivyosimamia utekelezaji wa zoezi la uandikishaji wa daftari l a orodha ya wapigakura kwa ajili ya Uchagzu wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini Septemba 27,2024.
Mwenyekiti wa Umoja huo, Ramadhani Kasongo amesema wakati zoezi likiendelea wamefanikiwa kutembelea kwenye halmashauri na kujionea hali ya utekelezaji wa zoezi hilo, ambapo wameridhishwa na ushirikishwaji mkubwa wa vyama vya siasa katika maamuzi yaliyokuwa yakifanywa na watendaji wa Serikali katika kufanikisha zoezi hilo.
Amesema mafani kio mengine waliyoyashudia wakati zoezi hilo likiendelea ni pamoja na mawakala kushiriki zoezi hilo kwa Amani sambamba na kutawala kwa uwazi katika maamuzi yaliyokuwa yakifanyika.
Aidha Kasongo ametoa wito kwa wanachama wa vyamba vya Siasa pamoja na wasimamizi wa uchaguzi kuendelea kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za uchaguzi ili kudumisha Amani na utulivu jambo litakalochangia kuwapata viongozi bora na wenye dhamira ya kuliletea Taifa Maendeleo.
Upande wake Katibu wa Chama cha NCCR-Mageuzi mkoa wa Kigoma Rajabu Hamis ametoa wito kwa makatibu wa vyama vya Siasa mkoani Kigoma kuendelea kushiriki kikamilifu katika kutoa hamasa , kusimamia maadili ya vyama na kufuatilia hatua zote kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ili kuwapa taarifa wanachama wenzao, jambo litakalochangia kuondoa sintofahamu zinazojitokeza ndani ya vyama vyao.
Niwasisitize viongozi wenzangu wa vyama vya siasa kushiriki siasa safi kwa kuacha kuendekeza tetesi katika utendaji kazi wao bali wazingatie taratibu za uchaguzi na kudumisha upendo miongoni mwetu viongozi wa kisiasa na wananchi tunaowaongoza.
Naye Musa Habib ambaye ni Katibu wa Chama cha ADA TADEA Mkoa wa Kigoma amesema viongozi wa Umoja wa vyama vya Siasa Mkoa waliamua kukagua maendeleo ya zoezi la uandikishaji daftari la wakazi ili kujiridhisha na kuona namna zoezi hilo linavyofanyika na kutoa ushauri kwa wasimamizi ili kuondoa dosari ndogondogo zilizokuwa zikijitokeza.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa