Jumla ya vijiji 270 kati ya 306 vya Mkoa wa Kigoma vimefikiwa na huduma ya Maji ikiwa ni sawa na 70.4% ya upatikanajinwa huduma hiyo ambapo kati ya hivyo 48 vinatumia visima pamoja na chemichemi zilizoboreshwa.
Akizungumza kupitia kipindi cha 360 cha Clouds TV, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye amesema kwa upande wa mjini, Mamlaka ya Maji imefikisha huduma hiyo kwa Asilimia 92 kwa Mji wa Kigoma, 78% Mji wa Kasulu huku Kibondo ikiwa 72.6% ambapo kwa vijijini huduma hiyo imefikia 70.4%.
Amesema Kuanzia Machi 2021 Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu imeelekeza kiasi cha Shilingi Bil. 96 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maji mkoani Kigoma ambapo upande wa mjini zimetolewa Shilingi Bil. 45 na vijijini Bil.51.
Amefafanua kuwa, kuanzia Machi 2021 hadi kufikia Oktoba 2024, jumla ya miradi 56 imetekelezwa na kukamilika katika maeneo ya mjini na vijijini kwa gharama ya Shilingi Bil. 75.
Amesema jumla ya Miradi 29 yenye Thamani ya Shilingi Bil. 78 inaendelea kutekelezwa ili kuongeza kiwango cha upatikanaji wa huduma hiyo mkoani Kigoma.
Aidha katika kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kwa ubora na uhakika Mhe. Andengenye amesema kuanzia Julai 2024 serikali iliweka mpango wa kuchimba visima 30 kwenye vijiji vyote vyenye changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji ambapo mpaka kufikia Oktoba 2024 visima 15 vimeshachimbwa na kuanza kutoa huduma.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa