Jumla ya vifaa Tiba 38 vyenye Thamani ya Shilingi 214,253,955.11 vilivyotolewa na Serikali ikiwa ni kati ya vifaa vilivyotolewa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu mara baada ya kufanya uzinduzi wa vituo 16 vya kutolea huduma ya Afya.
Akitoa Taarifa kwa Umma kuhusu mapokeai ya vifaa hivyo vilivyotolewa katika Kituo cha Afya Bunyambo kilichopo Halmashauri ya wilaya ya Kibondo, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye aesema upatikanaji wa vifaa hivyo umelenga kuwezesha upatikanaji wa Huduma ya upasuaji wa dharura kwa kina mama wajawazito.
Amevitaja vifaa hivyo kuwa ni mashine ya usingizi, mashine ya kukausha nguo, meza ya upasuaji, taa za uchunguzi, vitakasa vifaa, majokofu ya kutunzia damu na dawa, vifaa vya kuratibu mapigo ya moyo, vifaa vya upasuaji, kusaidia upumuaji na vile vya uchunguzi kwa mama wajawazito.
Kupitia taarifa yake, mkuu huyo wa Mkoa amewakumbusha watendaji wa Idara ya Afya kuendelea kutunza vifaa hivyo ili viweze kuwanufaisha wananchi kimatibabu kwa muda mrefu kwani serikali inaingia gharama kubwa kununua vifaa tiba hivyo.
Upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Jesca Lebba amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kuidhinisha kupatikana kwa vifaa hivyo kwani wakazi wa eneo hilo walikuwa na uhitaji mkubwa wa vifaa tiba hivyo.
Amesema pamoja na upatikanaji wa vifaa hivy, bado mkoa unachangamoto ya utoshelevu wa Ikama ya wahudumu wa Afya kwa Asilimia 67 hali inayochangia kuendelea kuwepo kwa changamoto ya utoaji wa huduma kwa asilimia mia moja.
Katika kukabiliana na changamoto hiyo Dkt. Lebba amesema tayari kwa kushirikiana na mamlaka za Ajira, mkoa umefanikiwa kutoa nafasi za wayendaji wa kujitolea zaidi ya 1000, kutumia huduma ya mama msindikizaji pamoja na uwepo wa fursa ya watendaji katika vyuo vya kutolea huduma za Afya.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa