MHE. JAJI RUFAA JACKOBS MWAMBEGELE MWENYEKITI WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI WAKATI AKITOA TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUSOGEZWA KWA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU WAPIGA KURA MKOANI KIGOMA LEO JUNI 22, 2024 KATIKA UKUMBI WA MANISPAA YA KIGOMA UJIJI MJINI KIGOMA.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza kusogezwa mbele kwa Zoezi Maalum la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura ambalo lilitarajiwa kuanza Julai Mosi hadi 7, 2024 ambapo sasa litafanyika tarehe 20-26 Julai 2024, uzinduzi wake kitaifa utafanyika Mkoani hapa.
Akitoa Taarifa kwa Umma kupitia vyombo vya Habari Mkoani Kigoma, Mwnyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Mhe. Jaji Rufaa Jackobs Mwambegele amesema Tume imezingatia maoni yaliyotolewa na wadau na kufikia maamuzi hayo ya kusogeza mbele zoezi la uboreshaji wa Daftari hilo.
Amefafanua kuwa, taratibu za awali kuhusu utekelezaji wa zoezi hilo zitabaki kama zilivyopangwa ambapo Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa(Mb)
Aidha Jaji Rufaa Jackob Mwambegele amewataja wadau waliokutana na Tume kisha kushiriki kutoa maoni kuwa ni pamoja na Viongozi wa Vyama vya Siasa, Viongozi wa Dini, wawakilishi Asasi za kiraia, wahariri wa vyombo vya Habari, waandishi wa Habari, Maafisa Habari, wawakilishi wa Makundi mbalimbali ya vijana, watu wenye ulemavu, wanawake na wazee wa kimila.
Aidha ameendelea kufafanua kuwa kwenye mikutano na wadau hao wameshauri kuwa, Taasisi na Asasi zilizoomba kibali cha kutoa Elimu ya mpiga kura wakati wa uboreshaji wa daftari, zinahitaji kuongezewa muda utakaowawezesha kupata fedha kutoka kwa wafadhili kwa ajili ya kuwawezesha kutekeleza majukumu yao.
Pili taasisi zenye kibali cha kuwa waangalizi wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo kuomba kuongezewa muda ili ziweze kupata fedha kutoka kwa wafadhili kwa ajili ya kufanikisha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Tatu, vyama vya Siasa vilitoa maoni kuhusu uhitaji wa kupatiwa muda wa kutosha kwa ajili ya kuwapata mawakala sambamba na kutoa Elimu kwa Wananchi ili waweze kujitokeza na kushiriki zoezi hilo.
Aidha wadau hao walishauri tume ijipe muda wa kutosha kwa ajili ya kutoa Elimu ya mpiga kura kwa wadau na wananchi kabla ya kuanza kwa zoezi hilo ili waweze kujitokeza kwa wingi na kushiriki.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa