MKUU WA MKOA WA KIGOMA THOBIAS ANDENGENYE (KULIA) AKIZUNGUMZA MARA BAADA YA KUKARIBISHWA NA MCH. DKT. BONIFACE MWAMPOSA WA MADHABAHU YA INUKA UANGAZE, KWA AJILI YA KUTOA SALAMU ZA SERIKALI KWA WAUMINI WALIOJITOKEZA KATIKA UWANJA WA KAWAWA MANISPAA YA KIGOMA UJIJI KWA AJILI YA KUPATA NENO LA MUNGU NA HUDUMA YA MAOMBEZI (UPAKO)
Hali ya ukosefu wa utii na hofu ya Mungu inayosababishwa na baadhi ya watu kutosimama katika misingi ya kiimani imeelezwa kuchabgia kwa kiasi kikubwa uwepo wa Imani za kishirikina kwa baadhi ya wanajamii mkoni Kigoma.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye alipozungumza wakati aliposhiriki Maombi na Ibada iliyoongozwa na Mchungaji Dkt. Boniface Mwamposa katika uwanja wa Kawawa, Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani hapa.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kutokana na baadhi ya wanajamii kushindwa kuzingatia mafundisho yanayotolewa kuendana na miongozo ya dini zao, wameendelea kujikuta wakishiriki vitendo ambavyo ni kinyume na matakwa ya dini hizo na kusababisha ukosefu wa Amani katika jamii.
Upande wake Mchungaji Mwamposa kupitia mahubiri yake amesema viongozi wa kiroho bado wanajukumu kubwa la kuwaombea waumini wao ili kuwabadilisha na kubaki katika muelekeo wa kweli katika kumuamini Mungu.
Aidha Mwamposa amempongeza Mkuu huyo wa Mkoa pamoja na viongozi wengine wa kiserikali kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa viongozi wa dini ikiwemo yeye mwenyewe na kusisitiza kuendelea kuwaombea viongozi hao ili wazidi kutekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa.
‘’viongozi wa Serikali mnaposhiriki nasi mnatufanya tuendelee kuaminiwa na wananchi lakini pia kuonesha umoja wetu katika utekelezaji wa majukumu kuendana na namna ambavyo Mungu amempangia kila mwanadamu’’ amesema Mwamposa.
Aidha Mwamposa ameiasa Jamii kuchana na Ramli chonganishi pamoja na kutegemea nguvu za giza kwa kudhani kuwa, ushirikina ni chanzo cha mafanikio.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa