Kupitia Programu ya uboreshaji wa Elimu Sekondari (SEQUIP) Juni 30, 2023 Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma ilipokea kiasi cha Shilingi 603,890,562/= kwa ajili ya ujenzi wa Miundombinu ya Shule ya Sekondari Nkungwe iliyopo kata ya Mkungwe iliyopo katika Halmashauri hiyo.
Mapokezi ya Fedha hizo yalilenga kutekeleza ujenzi wa miundombinu ya shule hiyo ikiwemo vyumba vine vya madarasa, Jengo la Utawala, majengo ya Maabara za Kemia, Fizikia, Baiolojia, Jengo la Maktaba, TEHAMA, Matundu kumi (10) ya Vyoo, Tenki la Maji na kichomea taka.
Mpaka kufikia Machi Mosi, 2024, majengo ya madarasa yamekamilika na yameshaanza kutumika, majengo ya Maktaba na lile la TEHAMA ujenzi wake umekamilika na kilichobaki ni marekebisho madogo hususani mifumo ya umeme, majengo ya maabara yamekamilika na yako tayari kuanza kutumika, ujenzi wa vyoo umekamilika sambamba na jengo la utawala ambalo marekebisho madogo ya mifumo ya umeme yanaendelea kukamilishwa.
Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Yusuf Makoko ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kutoa Fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo ambayo kukamilika kwako kutakuwa Mwarobaini wa kuondoa utoro na kuongeza mwamko wa Elimu katika Kata ya Nkungwe kutokana na wahitimu wengi wa darasa la saba kusoma katika shule hiyo iliyopo jirani na makazi yao.
Makoko amesema uwepo wa miundombinu bora utachangia kwa kiasi kikubwa kwa walimu na wanafunzi kushiriki kwa ufasaha matendo ya ufundishaji na ujifunzaji jambo litakalochangia kuinua Taaluma katika Shule hiyo na Mkoa kwa ujumla.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule hiyo, wameuomba Uongozi wa Halmashauri hiyo kuboresha miundombinu ya barabara iendayo shuleni hapo ili kuwaondolea adha ya uwepo wa tope na utelezi nyakati za masika.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa