Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungno wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema Seriali ya Tanzania itasimamia na kuhakikisha mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Uvinza hadi Msongati Burundi Km. 240 unakamilika kwa wakati.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye uzinduzi wa ujenzi wa Reli hiyo nchini Burundi Agosti 16,2025 na kusisitiza kuwa reli hiyo itasaidia usafirishaji wa rasilimali za kiuchumi ikiwemo madini aina ya Nikel, kutoka nchini humo hadi Bandari ya Dar Es Salaam.
Amesema mradi huo ambao utachukua kipindi cha miaka mitano kukamilika sambamba na mwaka mmoja wa uangalizi, itakuwa ndio reli ya kwanza kuunganisha nchi na nchi katika ukanda wa Afrika mashariki huku ukiimarisha shughuli za kibiashara, mahusiano na ustawi wa jamii baina ya nchi mbili za Tanzania na Burundi.
"Kwa sasa maroli yanatumia saa 96 kutoka Dar es Salaam hadi Bujumbura huku usafirishaji mizigo ukitarajiwa kutumia saa 20 tu baina ya maeneo hayo mara baada ya ujenzi wa miundombinu hiyo kukamilika" amesema Waziri Mkuu.
Amesema Serikali itaendelea kutoa maelekezo kwa Wizara pamoja na Bodi ya wakurugenzi na watendaji wa Shirika la Reli Tanzania ili kuhakikisha mradi unasimamiwa kwa usahihi ili uweze kukamilika kwa wakati na ubora.
Upande wake Rais wa Burundi Evarist Ndayishimiye ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuwa mshirika muhimu wa maendeleo ya nchi hiyo.
Aidha, ameushukuru uongozi wa Shirika la Reli nchini Tanzania (TRC) kwa kukubali kuwa mdau muhimu katika usimamizi wa mradi huo.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa