JENGO LA OFISI YA MKUU WA WILAYA YA KAKONKO LIKIWA KATIKA UJENZI AMBAPO LINATARAJIWA KUKAMILIKA IFIKAPO DESEMBA 2025.
Mradi wa ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kakonko unakaribia kukamilika ifikapo Desemba 2025 na kuruhusu kuanza kutumika kwa ofisi mbalimbali za watendaji ndaji ya jingo hilo.
Mhandisi Mkuu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Francisco Magoti anasema ujenzi wa mradi huo utagharimu kiasi cha Shilingi Bil1.6 hadi kukamilika kwake, huku akifafanua kwamba kazi zilizobaki katika utekelezaji ni pamoja na kufanya msawazo wa ardhi katika eneo la jingo, ujenzi wa nyumba ya mlinzi pamoja na uzio.
Magoti amesisitiza kuwa, faida ya mradi huo ni pamoja na kuboresha mazingira ya kutoa na kupokea huduma kwa wananchi wa Kakonko pamoja na kutoa fursa za ajira ya muda kwa wananchi wa eneo unapotekelezwa mradi huo.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa