• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko / Mrejesho |
KIGOMA   REGION
KIGOMA   REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Kigoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Seksheni ya Elimu
      • Seksheni ya Afya
      • Seksheni ya Miundombinu
      • Seksheni ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Mipango na Uratibu
      • Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Fedha
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwami
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Kibondo
      • Halmashauri ya Kibondo
    • Wilaya ya Kigoma
      • Halmashauri ya Kigoma
      • Manispaa ya Kigoma Ujiji
    • Wilaya ya Kakonko
      • Halmashauri ya Kakonko
    • Wilaya ya Kasulu
      • Halmashauri ya Kasulu
      • Halmashauri ya Kasulu Mji
    • Wilaya ya Uvinza
      • Halmashauri ya Uvinza
    • Wilaya ya Buhigwe
      • Halmashauri ya Buhigwe
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Kigoma Ujiji
    • Halmashauri ya Buhigwe
    • Halmashauri ya Kasulu
    • Halmashauri ya Kasulu Mji
    • Halmashauri ya Kibondo
    • Halmashauri ya Uvinza
    • Halmashauri ya Kakonko
    • Halmashauri ya Kigoma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Kigoma Special Economic Zone
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mikakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Picha

TUZIBADILI CHANGAMOTO KUWA FURSA ILI KUBORESHA ELIMU KATIKA MKOA WETU-NDIGEZA

Posted on: January 10th, 2023

Wadau wa Elimu mkoani Kigoma wametakiwa kuzibadili changamoto kuwa fursa kwa kutanguliza uzalendo na kudumisha weledi katika kutekeleza mikakati mbalimbali inayoandaliwa na Serikali ili kuboresha na kuinua kiwango cha Elimu.

Wito huo umetolewa na Kaimu Katibu Tawala Msaidizi upande wa Elimu Mkoa wa Kigoma Paulina Ndigeza, alipokuwa anafungua Kikao kazi cha Utiaji Saini Mkataba wa Utendaji Kazi baina yake na Maafisa Elimu Sekondari kilichofanyika wilayani Kasulu Mkoani hapa.

Ndigeza amesema kuwa dhamira ya Serikali kupitia mkataba huo ni kuhakikisha yanafanyika maboresho makubwa katika Sekta ya Elimu ili kuimarisha hali ya utendaji kazi katika mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji ili kuinua kiwango cha Elimu sambamba na ufaulu nchini.

Serikali inawekeza kiasi kikubwa cha Fedha katika kukabili changamoto na kuboresha miundombinu ya Elimu nchini. Hivyo watendaji wameshauriwa kufanya kazi kwa weledi ili kurejesha thamani ya Fedha ambayo Serikali inaendelea kuwekeza katika Sekta ya Elimu.

Aidha Ndigeza amesisitiza Maafisa Elimu Sekondari kwenda kusimamia vigezo vyote 22 vya upimaji wa utendaji kazi vilivyoainishwa kwenye mikataba waliyoisaini ili kuleta matokeo chanya kwa kuongeza ufaulu katika matokeo ya mitihani ya kuhitimu  Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Sita.

Naye Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Kibondo Julius Kakiama, amesema vigezo vilivyomo kwenye mikataba hiyo vitawaongezea ari  ya utendaji kazi kwani inatoa fursa ya kila mtendaji kujipima na kujitathimini kisha kujua mapungufu yake na hatua za kuchukua ili kutimiza malengo yaliyowekwa.

‘‘Unapokuwa na mwongozo kama huu uliomo kwenye mkataba unarahisisha  kufahamu majukumu unayopaswa kuyatekeleza na kutambua hatua uliyofikia kiutekelezaji hivyo kuruhusu uwezekano mkubwa wa kupata matokeo chanya’’ amesema Julius.

Upande wake Afisa Elimu Kata Ruben Kahuza amesema kupitia kikao hicho wamejifunza namna ya kuzibadili changamoto kuwa Fursa ili kuepuka sababu zozote zitakazosababisha kushindwa kutekelezwa kwa vigezo vya upimaji vilivyomo kwenye mkataba wa utekelezaji.

Pamoja na uwepo wa changamoto ya kutotosheleza kwa ikama ya walimu, umbali kutoka makazi hadi shule zilipo pamoja na uelewa duni wa baadhi ya wazazi kuhusu ushiriki wa masuala mbalimbali ya kielimu. Watendaji tunapaswa kuzibadili na kuzifanya fursa ili kuhakikisha malengo yaliyowekwa na Serikali ili kuinua ufaulu yanafikiwa.

MAKABIDHIANO YA  MIKATABA YA  UTENDAJI KAZI BAINA YA  AFISA ELIMU MKOA WA KIGOMA NA BAADHI YA MAAFISA ELIMU WA HALMASHAURI  ZA MKOA WA KIGOMA LEO JANUARI 10, 2023 WILAYANI KASULU.


Matangazo

  • MAZOEZI KWA AFYA YAKO March 23, 2017
  • UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024 September 12, 2024
  • UJIO WA MADAKTARI BINGWA MKOANI KIGOMA November 12, 2018
  • Fomu ya Usajili wa Maonesho TBS Kigoma May 01, 2022
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • RC ANDENGENYE AKABIDHI VITENGO VITENGO VYA LISHE MKOA NA WILAYA UVINZA

    May 09, 2025
  • DCP NARCIS MISSAMA AFANYA ZIARA MKOANI KIGOMA

    May 07, 2025
  • JAJI ASINA AKAGUA ZOEZI LA UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI-KIGOMA

    May 03, 2025
  • VYAMA VYA WAFANYAKAZI VISIGEUKE MAHAKAMA ZA KUWAHUKUMU WATUMISHI-RC ANDENGENYE

    May 01, 2025
  • Ona vyote

Video

RC ahimiza wananchi anuani za Makazi
Video nyingine

Tovuti zinazo fanana

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA BUHIGWE
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KAKONKO
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
  • HALMASHAURI YA MJI KASULU
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBONDO
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA
  • HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGOMA UJIJI
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA

Tovuti zinazo husiana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI PORTAL
  • IKULU
  • OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    MKOA WA KIGOMA

    Anuani: S.L.P 125

    Simu: 0282802330

    Simu ya kiganjani: +255766853404

    Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://bachelorthesiswritingservice.com

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa