Jamii mkoani Kigoma imetakiwa kuwaenzi Mashujaa na Waasisi wa Taifa la Tanzania kwa kuendelea kupambana dhidi ya Maradhi, Umasikini na Ujinga ili kuzidi kuliletea Taifa Maendeleo.
Akizungumza mara baada ya kuongoza zoezi la usafi wa Mazingira katika Hospitali ya Mkoa ya Maweni ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya kilele cha Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa nchini, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema kila mtu anawajibu wa kuongeza
Amesema jamii inapaswa kutambua wajibu wake katika kujikinga na Maradhi ili kunusuru Fedha zilizotengwa na Serikali kwa ajili ya kugharamia matibabu ziweze kuelekezwa katika utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
Pia ameitaka Jamii kukabiliana na Ujinga kwa kuhimiza na kuhakikisha watoto wote wanapata Elimu itakayowasaidia kukabiliana na mabadiliko katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo Duniani.
Aidha amesisitiza kuwa, wakazi wanapaswa kujibiidisha katika kufanya kazi ili kujiongezea kipato na kujikomboa dhidi ya wimbi la umasikini.
‘’Vita tunayopigana sasa atuhitaji kutumia Silaha bali ni vita ya kifikra ili kujikomboa na kufikia Malengo yetu kwa kukabiliana na maadui Ujinga, Umasikini na Maradhi’’ amesema Andengenye.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ameziagiza Halmashauri zote mkoani hapa kuhakikisha zinatekeleza agizo la Serikali la kutenga Siku moja kila Mwezi kwa ajili ya kufanya usafi wa Mazingira.
Amesema tabia hiyo inatakiwa kuimarishwa ili Jamii iweze kujenga Utamaduni wa uwajibikaji binafsi katika kutunza Mazingira na kujikinga na Maradhi.
Zoezi hilo limehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Kamati ya Usalama Mkoa, Wakuu wa Idara na Sehemu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi wa Manispa ya Kigoma Ujiji na Halmashauri ya Kigoma Vijijini, Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mkoa Maweni pamoja na watumishi mbalimbali wa Serikali.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa