Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye amesema ataendeleza ushirikiano na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Jane Goodall katika masuala ya Ulinzi na Uhifadhi wa Mazingira mkoani hapa.
Mkuu wa Mkoa amesema hayo Leo tarehe 29 Julai 2022, alipotembelewa na Dkt. Jane Goodall ambapo amepokea taarifa ya kazi zinazofanywa na Taasisi hiyo mkoani Kigoma na kuahidi ushirikiano kwenye Programu ya uhifadhi wa mazingira asilia na utafiti wa Tabia za Wanyama aina ya Sokwe kwenye hifadhi ya Taifa ya Gombe mkoani hapa.
Aidha Mkuu wa Mkoa amesema kwa kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama, wataendelea kuimarisha usalama katika hifadhi ya Gombe ili kudumisha kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Taaisisi hiyo.
Kwa Upande wake Dkt. Kasukula Nyamaka ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Program ya uhifadhi wa Mazingira katika Taasisi ya Jane Goodall Tanzania, amesema lengo la ziara hiyo ni kumtambulisha Dkt. Goodall kwa Mkuu wa Mkoa na kuwasilisha taarifa pamoja na mrejesho wa Kazi wanazozifanya katika mkoa wa Kigoma.
Taasisi ya Jane Goodall ilianzishwa nchini mwaka 1977, ikiwa na lengo la kufanya utafiti wa tabia za wanyama aina ya Sokwe, ulinzi wa Mazingira na kuboresha Uchumi wa Jamii kwa kutumia maliasili zinazowazunguuka.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa