Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mhe. Thobias Andengenye akitoa hotuba kwa wajumbe wa Kikao cha Ujirani Mwema( hawapo pichani) wakati akifungua Kikao hicho kilichofanyika katika Ukumb wa Kigoma Social Hall Mjini hapa.Mkuu wa Mkoa wa Makamba nchini Burundi Bi. Francoise Ngozirazana akitoa neno mara baada ya ufunguzi wa Kikao hocho cha Ujirani mwema.
Baadh ya wajumbe wa Mkutano wa Ujirani mwema kutoka nchini Burundi wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma( hayupo pichani)
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mhe. Thobias Andengenye amesema Mkoa utaendelea kushirikiana na uongozi wa mikoa ya nchi ya Burundi inayopakana na Mkoa wa Kigoma ili kuimarisha usalama na mahusiano mema ajili ya maendeleo ya wananchi wa maeneo hayo.
Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua Mkutano wa Ujirani Mwema kati ya Tanzania na Burundi kwa Mikoa inayopakana na Mkoa wa Kigoma kilichoanyika leo tarehe 17. Novemba 2022 katika Ukumbi wa Kigoma Social Hall uliopo mjini hapa.
Amesema Uongozi wa Mkoa wa Kigoma unaendelea kutumia fursa ya vikao vya Ujirani mwema kwa ajili ya kupeana mikakati ya kuimarisha usalama katika maeneo ya mpakani ili kuimarisha utulivu na kutoa fursa kwa wananchi kushiriki shughuli mbalimbali za uzalishaji Mali.
‘’kupitia kikao hiki, Tujadili changamoto zinazowakabili Wananchi wetu kisha tuzitafutie ufumbuzi na kuhakikisha maazimio mbalimbali tunayoazimia hapa tunayatekeleza ili kuondoa kero zinazowakabili wananchi wetu ili waweze kuishi kwa amani na utulivu’’ Amesema.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Makamba Francoise Ngozirazana ambaye pia ni kiongozi wa msafara huo, amesema vikao hivyo vimeendelea kuleta tija na matokeo chanya ikiwemo kuimarisha hali ya utulivu na amani nchini Burundi.
‘’Kwa sasa wakimbizi wanaendelea kurejea nchini kutokana na kuimarika kwa hali ya usalama na kuruhusu wananchi kuendelea na shughuli zao za uzalishaji mali bila kuwepo kwa usumbufu wowote’’
Mwandishi wa Habari wa shirika la utangazaji la Taifa Burundi (ABP) Alain Bucumi aliyeongozana na msafara huo, amesema kudumisha kwa mahusiano ya nchi hizo mbili ni muhimu kwa sababu Tanzania imeendelea kuwa kitovu cha shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa nchi ya Burundi.
Aidha, amewaasa wakazi kutoka nchini hiyo jirani kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria na kuepuka vitendo visivyo vya kimaadili wanapopata fursa ya kuingia nchini Tanzania kwa malengo ya kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ili waweze kutimiza malengo yao.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa