Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye amewataka wataalam wa Serikali na Sekta binafsi, kutumia takwimu zitakazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) katika kupanga na kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo mkoani hapa, kufuatia kukamilika kwa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi kwa Mwaka 2022.
Mkuu wa Mkoa ametoa Rai hiyo wakati akifungua Kikao cha Tathimini ya Zoezi la Sensa kwa Mkoa wa Kigoma kilichofanyika Leo Tarehe 24 Oktoba 2022, ambapo pamoja na mambo mengine ametoa pongezi kwa Kamati za Sensa ngazi zote, viongozi wa Madhehebuya Dini, waandishi wa Habari pamoja na wananchi wa Mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na kuhakikisha zoezi hilo limefanyika na kukamilikwa kwa mafanikio makubwa.
‘‘Wataalam wa Idara za Afya, Elimu, uchumi, Mipango, nk mnaotekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, mkazitumie takwimu hizo mpya marazitakapotolewa na Serikali kama miongozo katika mipango ya utekelezaji wa majukumu yenu ili mfanye kazi kwa ufanisi na kupata matokeo chanya’’ amesema Andengenye.
Naye Meneja wa Takwimu Mkoa wa Kigoma, Moses Kahero amesema taarifa za Sensa ya Watu na Makazi kwa Mwaka 2022 zitakapotangazwa Rasmi, zitatoa picha kamili kuhusu hali ya mgawanyo wa huduma za Serikali kwa jamii na kuonyesha maeneo yanayohitaji kufanyiwa maboresho ili kuendana na hali halisi ya mahitaji.
Kahero ameitaja changamoto ya uwepo wa wananchi katika maeneo yasiyo rasmi kimakazi hususani maeneo ya Hifadhi za Misitu, ilichelewesha zoezi la hilo la Sensa na kusisitiza kuwa, juhudi zilifanyika na wakazi hao walifikiwa kisha kuhesabiwa.
Aidha ameushukuru uongozi wa Mkoa kwa kushirikiana na viongozi wengine wa Serikali, Taasisi binafsi pamoja na wadau mbalimbali wa Mendeleo kwa kufanikisha zoezi hilo muhimu kwa maendeleo ya Taifa.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa