Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema ushiriki wa Timu ya Mashujaa katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara utatia chachu katika Maendeleo ya Uchumi wa Mkoa wa Kigoma.
Andengenye ametoa kauli hiyo, alipotembelea na kukagua maendeleo ya ukarabati wa uwanja wa CCM Lake Tanganyika utakaotumiwa na Timu ya Mashujaa FC ya Mkoani Kigoma kwa Michezo ya Nyumbani katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara Msimu wa 2023/2024.
Amesema kuwa, kutokana na Ushiriki wa Timu hiyo Mkoa wa Kigoma utapokea wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kushuhudia Michezo ya Ligi kuu, ambapo wafanyabiashara mbalimbali watapata fursa ya kunufaika kiuchumi kutokana na kuwahudumia wageni hao.
‘’Pamoja na kupata Burudani kupitia michezo, pia kuna fursa mbalimbali za kibiashara zitakazoweza kutuimarisha kiuchumi, hivyo nitoe wito kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo mkoani hapa kuchangamkia Fursa hii ya ujio wa wageni kwa ajili ya kufanya biashara mbalimbali zitakazowaimarisha kiuchumi.
Upande wake Katibu Tawala Msadidi, Miundombinu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Francisco Magoti, amesema ukarabati huo unafanyika katika Sehemu za Majukwaa, vyumba vya kubadilishi mavazi kwa wachezaji, vyoo, Ukumbi mdogo wa ndani ya Uwanja pamoja na eneo la kuchezea Mpira.
‘’Tutahakikisha zoezi hili la maboresho ya maeneo muhimu ya uwanja linakamilika kabla ya kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ili kuruhusu michezo ifanyike kama ilivyopapangwa’’ amesisitiza Magoti.
Upande wake Afisa Vijana Mkoa wa Kigoma Edward Manase amewasisitiza watendaji pamoja na wasimamizi wa uwanja huo kuzingatia ubora katika zoezi hilo la ukarabati wa uwanja huo.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa