Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amewaelekeza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa mkoani hapa, kutumia Asilimia Arobaini ya Makusanyo ya ndani kutekeleza miradi itakayosaidia kurahisisha upatikanaji wa Huduma za jamii kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa ametoa kauli hiyo alipozungumza na Madiwani kupitia Mikutano Maalum wa Baraza la Madiwani katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, uliolenga kujadili hoja na Mapendekezo ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 na kusisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuona matokeo ya fedha wanazochangia serikali kupitia kuimarishwa kwa hali ya upatikanaji wa huduma.
‘’Miradi inayotekelezwa isiishie kwenye makaratasi bali ipimwe na wananchi kwa kuonekana huku ikitoa matokeo ya moja kwa moja katika kutatua shida na kuleta suluhisho dhidi ya kero mbalimbali zinazowakabili wananchi katika maeneo ya Halmashauri’’ amesema.
‘’Tuhakikishe fedha zinazokusanywa kupitia mapato ya ndani zinawarudia wananchi kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo ujenzi au kufanyika kwa maboresho kwenye miundombinu ya kielimu, Afya, Maji, nk’’ amesisitiza Andengenye.
Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa amesisitiza umuhimu wa Suala la kutoa Huduma ya chakula Shuleni ili kudhibiti utoro sambamba na kuimarisha Afya za wanafunzi.
‘’Wazazi wamekuwa wakitumia muda mwingi kufanya shughuli za kilimo maeneo ya mashambani na kushindwa kupata fursa ya kuwahudumia chakula watoto wao hivyo iwapo watoto hao watapatiwa chakula shuleni itawaounguzia adha ya kushinda bila kula kwa muda mrefu’’ amesisitiza Rugwa.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa