MKUU WA MKOA WA KIGOMA IGP MSTAAFU BALOZI SIMON SIRRO AKISALIMIANA NA BALOZI WA BURUNDI KATIKA UBALOZI MDOGO WA NCHI HIYO MKOA WA KIGOMA, KEKENWA GEREMIAH BAADA YA BALOZI HUYO WA BURUNDI KUMTEMBELEA MKUU WA MKOA KWA LENGO LA KUMSALIMIA NA KUJITAMBULISHA LEO AGOSTI 12,2025.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amesema Serikali ya Tanzania kupitia uongozi wa Mkoa wa Kigoma itaendelea kushirikiana na nchi ya Burundi kukuza Sekta za Biashara, Utalii na Uwekezaji ili kuimarisha uchumi wa nchi hizo mbili pamoja na kuwaletea Maendeleo wananchi katika maeneo hayo.
Balozi Sirro ametoa kauli hiyo alipofanya mazungumzo mafupi na Balozi katika Ofisi ya Ubalozi mdogo wa Burundi Mkoa wa Kigoma, Kekenwa Geremiah Leo Agosti 13, 2025 ambapo balozi huyo amemtembelea mkuu huyo wa Mkoa kwa lengo kumsalimia na kujitambulisha.
Amesema wakazi wa Burundi wanayo fursa ya kuwekeza katika mkoa wa Kigoma kutokana na kuimarika kwa Miundombinu ya Uchukuzi na uwepo wa Nishati ya Umeme ya uhakika kutokana na mkoa kuunganishwa na Umeme wa Gridi ya Taifa.
Kupitia mazungumzo yao wawili hao wamekubaliana kuendelea kudumisha vikao vya ujirani mwema sambamba na kuimarisha usalama katika maeneo ya mipaka ili kuruhusu wananchi kuishi kwa amani na utulivu jambo litakaloendelea kuchochea Maendeleo ya wakazi katika Mkoa wa Kigoma na mikoa jirani ya Burundi.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa