Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brig. Gen. Emmanuel Maganga emewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Kigoma kuwa Serikali ya Mkoa inafanya kila juhudi kuahikisha wananchi waliokidhi sifa za kupata Vitambulisho wanapata hadi kufikia mwezi Desemba 2019.
Ameyasema hayo wakati akizindua duka Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo Mkoani humo, amesisitiza kuwa kwakuwa suala la mawasiliano kwa sasa ni muhimu, ni wazi kuwa kila mtumiaji wa simu anapaswa kuwsajiliwa ili aweze kutumia kadi ya simu, hii ni kutokana na usalama wa mtumiaji na usalama wa nchi pia.
amesema anatambua kuwa kati ya mikoa ambayo bado wananchi wake hawajapata namba au vitambulisho vya Taifa, seriakli inafanya juu chini kukamilisha mchakato huo ili mwananchi anayestahili aweze kupata huduma hiyo.
ameonya kuwa watu wasilichukulie suala hili kuwa la kisiasa bali linamaslahi mapana ya Mkoa na Taifa kwa ujumla hivyo waache kuishinikiza serikali iharakishe kutoa vitambulisho ili watu wasio raia wapate upenyo wa kupewa vitambulisho vya taifa.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa